Posted by Esta Malibiche on Nov 26,2016 in NEWS
Naibu Waziri Ofisi ya Rais
TAMISEMI Selemani Jafo akisaini kitabu cha wageni shule ya sekondari
Segera, kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya
Handeni Bw. Wiliam Makufwe na kulia ni Mkuu wa Wilaya ya Handeni Mh.
Godwin Gondwe.
Picha ya pamoja ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tamisemi Selemani Jafo na walimu wa shule ya sekondari ya Segera.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Handeni William Makufwe akitoa utambulisho mfupi kwenye ukumbi wa Halmashauri.
Baadhi ya watumishi wa halmashauri ya Handeni
Viongozi wakisikiliza kwa makini maagizo ya Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Selemani Jafo.
………………………………………………………………………….
Naibu Waziri wa Nchi, Ofisi ya
Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI),SelemanI Jafo
amewataka maafisa elimu kupanga muda wa kusikiliza kero za walimu na
kuzitafutia ufumbuzi ili kuongeza morali ya walimu kufundisha.
Jafo ametoa agizo hilo alipokuwa
akiongea na walimu wa shule ya sekondari Segera iliyopo wilayani
Handeni, katika ziara yake aliyoifanya Wilayani Handeni na Mkoa wa
Tanga.
Amesema wapo baadhi ya Maafisa elimu ambao wanajifanya kuwa ni
Miungu watu linapokuja suala la kusikiliza na kutatua kero za walimu.
“Najua wapo wapo walimu
wanaotembea umbali mrefu kufuata huduma makao makuu ya Halmashauri kwa
wakubwa wao mara nyingi wameshindwa kutatuliwa kero zao hali
inayopelekea usumbufu, Kuanzia leo napiga marufuku tabia hiyo,”amesema
Jafo.
Amesisitiza Maafisa elimu hao
wapo kwa lengo la kuwasikiliza walimu na kuwasaidia kutatua kero zao ili
waweze kujikita katika ufundishaji wa wanafunzi.
Kadhalika, amebainisha walimu ni watu muhimu sana nchini ila wamekuwa wakikatishwa tamaa na utendaji wa baadhi ya maafisa elimu.
Ameongeza kuwa kero kubwa ya
walimu ni kutokupanda madaraja kwa wakati na kutopata stahiki zao ikiwa
ni pamoja na posho za likizo,uhamisho na madai mengine.
Katika hatua nyingine, Naibu Waziri Jafo ameagiza
Halmashauri ya Wilaya ya Handeni kukamilisha miradi yote ya SEDP-II
ambayo haijakamilika kuhakikisha inakamilika kabla au ifikapo desemba
20, mwaka huu.
“Katika kusimamia miradi hiyo na
miradi ya maendeleo kwa ujumla kila mtu lazima atimize wajibu wake na
kuhakikisha fedha iliyotengwa na kutolewa inatumika vizuri na thamani
fedha (value for money) inaonekana,”amesema Naibu Waziri Jafo.
0 maoni:
Chapisha Maoni