Posted by Esta Malibiche on Nov 16,2016 in NEWS
Naibu
Waziri (OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu
wenye Ulemavu, Dk. Abadallah Posi, akizungumza wakati akizindua tamasha
la tano ya watu wenye ulemavu nchini, lililoanza leo kwenye Hoteli ya
Blue Pearl jijini Dar es Salaam. Tamasha hilo limeandaliwa kwa udhamini
wa Shirika lisilo la kiserikali la The Foundation of Civil Society.
Picha na Muhidin Sufiani
Mkurugenzi
wa Shiriki lisilo la Kiserikali la Foundation for Civil Society,
Francis Kiwanga, akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi kufungua
Tamasha hilo kwenye Hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam,leo. Picha
na Muhidin Sufiani
Katibu
Mtendaji wa SHIVYAWATA, Felician Mkude, akitoa utambulisho kwa mgeni
rasmi wakati wa ufunguzi huo. Picha na Muhidin Sufiani
Sehemu
ya washiriki wa Tamasha hilo wakimsikiliza Mgeni rasmi Naibu Waziri
(OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu wenye
Ulemavu, Dk. Abadallah Posi wakati akisoma hotuba ya ufunguzi wa Tamasha
hilo. Picha na Muhidin Sufiani
Sehemu
ya washiriki wa Tamasha hilo wakimsikiliza Mgeni rasmi Naibu Waziri
(OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu wenye
Ulemavu, Dk. Abadallah Posi wakati akisoma hotuba ya ufunguzi wa Tamasha
hilo. Picha na Muhidin Sufiani
…………………………………………………………………………..
Naibu
Waziri (OWM) anayeshughulikia sera, Bunge, Kazi Ajira, Vijana na watu
wenye Ulemavu, Dk. Abadallah Posi leo amezindua tamasha la tano ya watu
wenye ulemavu nchini, Tamasha lililoandaliwa kwa udhamini wa Shirika
lisilo la kiserikali la The Foundation of Civil Society, lililofanyika
katika hoteli ya Blue Pearl jijini Dar es Salaam.
Dk.
Posi amebainisha katika Tamasha hilo kuwa, serikali ipo karibu na watu
wenye ulemavu na kwamba sheria iliyopitishwa mwaka 2010, kuhusu watu
wenye ulemavu imepitishwa na kwamba ni jukumu la jamii nzima
kushirikiana katka kutoa haki sawa kwa wananchi wote wakiwemo walemavu.
Dk.
Posi alifafanua kuwa, changamoto zinazowakabili walemavu hapa nchini ni
nyingi lakini pia serikali inazitambua, inazichambua na inazifanyia
kazi kwa kadri uwezo unapopatikana.
Kabla
ya hotuba ya Mgeni Rasmi, Mkurugenzi Mtendaji wa The Foundation for
Civil Society, Fransis Kiwanga alifafanua kuwa, shirika analoliongoza
kwa kutambua umuhimu wa kuwawezesha walemavu hapa nchini, liliona ni
busara kuchangia kuwepo kwa tamasha hili na kwamba ni faraja kwa shirika
hili kuona maisha na hali ya walemavu hapa nchini inabadilika.
“Tunaipongeza
serikali kwa kazi kubwa inayofanya, tunaipongeza sana katika suala zima
la kupinga rushwa, Tunaipongeza katika kuhakikisha kunakuwepo
mabadiliko ya utendaji pamoja na utoaji huduma kwa wananchi,” Mkurugenzi
huyo alisema na kuongeza kuwa, shirika lake kwa kutambua haki
mbalimbali za walemavu na hali halisi ya maisha hapa nchini, linaiomba
serikali kuhakikisha kuwa inakuwa karibu na watu wenye mahitaji maalum
ili nao wajione kuwa ni raia wa daraja la kwanza katika nchi yetu.
Tamasha
hili linalounganisha wawakilishi wa watu wenye mahitaji maalum kutoka
pane zote za Tanzania, linafanyika kwa siku mbili na likihusisha
wawakilishi wapatao 150 kutoka katika mikoa yote nchini Tanzania na
linafanyika hapa jijini Dar es Salaam kwa siku mbili.
0 maoni:
Chapisha Maoni