Ushauri
huo umetolewa mjini Dodoma na wabunge wa Bunge hilo baada ya kuujadili
mkataba huo kwa kina kwa kutoa maoni yao ambapo wengi wameunga mkono
kutosainiwa kwa mkataba huo.
Baadhi
ya wabunge waliopata nafasi ya kutoa maoni yao katika mjadala huo ni
Mbunge wa Mtwara Vijijini(CCM) Mhe. Hawa Ghasia amemshauri Mhe. Rais Dkt
.John Pombe Magufuli kutosaini mkataba huo kwa kuwa mkataba huo una
hasara nyingi kwa taifa kuliko faida.
”Kwa
kuzingatia mkataba umeruhusu uingizaji na utoaji wa bidhaa huru na
ukizingatia hakuna nchi hata moja ya Ulaya ambayo Tanzania inapeleka
bidhaa zake hivyo mkataba huu hauna maslahi kwa watanzania”, alisema
Mhe. Ghasia.
Ameongeza
kuwa Tanzania sio nchi ya kwanza kutosaini mkataba huo kwani kuna nchi
kama Angola, Nigeria, na Gambia hazijasaini,ameongeza kuwa kama Tanzania
itakubaliana na mkataba huo utaua viwanda pamoja na biashara za
Tanzania.
Kwa
upande wake Mbunge wa Nzega Mjini Hussein Bashe amesema kuwa tatizo
lililopo katika mkataba huo ni kutoitambua nchi kama nchi na badala yake
kuangalia nchi zote kwa pamoja hivyo amewashauri wabunge kuhoji kuanzia
kwenye kiini cha tatizo.
“Kwa
kuwa kifungu cha 143 cha mkataba huo kinaruhusu kupeleka marekebisho,
naishauri Serikali yetu ipeleke marekebisho ya kupendekeza kila nchi
iingie mkataba kivyake kulingana na maslahi ya nchi yake”, alisema
Bashe.
Aidha,
Mbunge wa Mwibara (CCM) Mhe.Kangi Lugola amempongeza Mhe. Rais Magufuli
kwa kukataa kusaini mkataba huo kwani ni miongoni mwa mikataba mibovu
kati ya mikataba iliyowahi kuletwa nchini kutoka katika nchi za Ulaya.
“Kama
tukikubali kusaini mkataba huu nchi hii itakuwa dampo la bidhaa
mbalimbali za ajabu kutoka nje na hivyo kupelekea kushindwa kutimiza
dhamira ya nchi ya kuimarisha viwanda vyetu”, alisema Mhe. Lugola.
Naye,
Mbunge wa Mchinga (CUF) Mhe. Hamidu Bobali amesema kuwa mkataba huo
haufai kwa maslahi mapana ya taifa hili kwani unataka kuondoa ushuru kwa
bidhaa zinazoingia nchini wakati nchi ya Tanzania inaingiza bidhaa
nyingi kutoka nje kuliko kupeleka bidhaa nje ya nchi.
“Kama
tukikubali tukaondoa ushuru wa kuingiza bidhaa kutoka nje basi
tutapoteza mapato mengi yanayotokana na kuwepo kwa bandari pia
tunatakiwa tujiulize kama mkataba umeruhusu uingizaji na utoaji wa
bidhaa huru je nchi yetu ina bidhaa zinazokidhi vigezo vya kuingia
katika nchi za Ulaya?” , alihoji Mhe. Bobali.
Mhe.
Bobali ametoa rai kwa Serikali kuileta Bungeni mikataba mikubwa kama ya
gesi na madini kwa ajili ya kujadiliwa kwa kina ili kuepuka kusaini
mikataba isiyo na tija kwa Taifa.
Na Jacquiline Mrisho – MAELEZO, Dodoma
0 maoni:
Chapisha Maoni