Kampuni
inayotoa huduma ya usafirishaji wa anga Qatar Airways nchini Tanzania
imechangia madawati 100 katika shule ya msingi Chanzige B, iliyopo
wilayani Kisarawe, mkoani Pwani, ikiwa ni sehemu ya mradi wa kusaidia
juhudi za serikali kupitia mpango wa kuondoa uhaba wa madawati nchini
kwa shule za msingi pamoja na sekondari hii ni pamoja na sehemu ya
kurudisha shukrani kwa jamii.
Mkabidhiano
hayo yamefanyika katika viwanja vya shule hiyo leo Novemba, 14 katika
viwanja vya shule hyo ambayo pia yakihudhuriwa na viongozi mbalimbali
akiwemo mbunge wa Kisarawe na Naibu Waziri wa ofisi ya Rais Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa, Mh.Seleman Jafo aliyekuwa mgeni rasmi
pamoja, meneja wa Qatar airways Tanzania, Basek Haydar, wafanyakazi wa
Qatar na wawakiishi kutoka ofisi ya Doha pamoja na Dk. Amon Mkoga ambaye
ni mkurugenzi mtendaji wa taasisi ya Amon Mkoga Foundation, bodi ya
wakurugenzi, walimu wa shule hiyo, wazazi na wanafunzi.
Akizungumza
katika makabidhiano ya madawati hayo, Meneja wa Qatar Airways, Basek
Haydar amemwakikishia naibu waziri Jafo kuwa wataendelea na mpango wa
kusaidia jamii kwa kushirikiana na serikali ya Tanzania kuinua na
kuimalisha sekta ya elimu nchini.
Kwa
upande wake naibu waziri Jafo ameipongeza Qatar Airways kwa msaada huo
kwani umewezesha kupunguza kero kwa wanafunzi waliokuwa wakikaa chini,
hata hivyo amewaomba uongozi wa shule hiyo kuangalia uwezekano wa kugawa
madawati hayo shule jirani pale wanapoona panafaa kutokana na uhitaji
uliopo.
0 maoni:
Chapisha Maoni