Posted by Esta Malibiche on Nov 30 ,2016 In NEWS
Na Esta Malibiche
Iringa
Kiwango cha ufaulu wa mitihani ya
kumaliza Elimu ya Msingi 2016 Mkoani Iringa kimeongezeka kutoka wastani wa 82.8% mwaka 2015
hadi kufikia 99.5% mwaka 2016.
Akizungumza na wandishi wa Habari
katika ukumbi wa Siasa ni Kilimo uliiopo katika Halmashauri ya Wialaya ya
Iringa,Katibu Tawala wa mkoa wa Iringa Wamoja Ayubu alisema
Ayubu lisema ongezeko hilo ni
mafanikio makubwa ambayo yameufanya mkoa kushika nafasi ya 3 kitaifa kati ya
mikoa 26 ya Tanzania bara.
‘’’’Ongezeko la ufaulu linaleta
changamoto mpya ambayo kuwa na madarasa na madawati ya kutosha kwa idadi ya
wanafunzi wote.’’’Alisema Ayubu
Akichanganua matokeo hayo alisema
mwaka 2016 mkoa ulikuwa na watahiniwa 21,270 waliosajiliwa kufanya
mtihani, ambapo waliofanya mtihani walikuwa watahiniwa 21,177 ikiwa ni
sawa na 99.5% namwa 2015 waliofaulu mtihani ni watahiniwa 17,587 sawa na
82.8%.
‘’’’Halmashauri ya mji wa Mafinga
imeweza kuongeza kiwango cha ufaulu ambapo Mafinga imeweza kushika nafasi
ya nne kitaifa wakati Kilolo imeongeza ufaulu kutoka kwa 13%, Wilaya ya Iringa
kwa 12%.’’’’alisema Ayubu.
Kwa upande wake Afisa elimu wa mkoa
Richard Mfugale alisema mwaka huu hakukuwa na tuhuma zozote za udanganyifu wa
mitihani kama ilivyotokea miaka ya nyuma.
Mfugale alisema kuwa wanafunzi 413
hawakuweza kufanya mtihani kwa sababu mbalimbali ikiwemo utoro, vifo, ugonwa ,
mimba na kuhama.
Naye Mwenyekiti wa Halmashauri ya
wilaya ya Iringa Stevin Mhapa alisema wamefanikiwa kuongeza kiwango cha ufaulu
kutokana na kufuata ushauri uliotolewa kwenye kikao kama hicho kilichopita
sambamba na kufanya tathimini za mara kwa mara.
0 maoni:
Chapisha Maoni