Posted by Esta Malibiche on Nov 16,2016 in NEWS
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani)
mara baada ya kumaliza kikao chake na Menejimenti ya Mamlaka ya
Vitambulisho vya Taifa (NIDA) wakati alipofanya ziara ya kikazi Makao
Makuu ya NIDA, Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Mwigulu aliwaambia
waandishi wa habari kuwa, NIDA itaanza kutoa namba za utambulisho kwa
wananchi wote kuanzia mwezi Desemba mwaka huu, ambao wamesajiliwa
kupitia mpango wa usajili wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC). Kushoto ni
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka hiyo, Andrew Massawe. Picha zote na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe (watano kushoto)
akimuelezea jambo Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba
(katikati) wakati Waziri huyo alipotembelea Makao Makuu ya Mamlaka hiyo,
Kinondoni, jijini Dar es Salaam leo. Kiongozi huyo wa NIDA katika
hotuba yake fupi kwa Waziri Mwigulu, alisema kuwa, NIDA itaanza kutoa
namba za utambulisho kwa wananchi wote kuanzia mwezi Desemba mwaka huu,
ambao wananchi hao wamesajiliwa kupitia mpango wa usajili wa Tume ya
Taifa ya Uchaguzi (NEC).
Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi,
Mwigulu Nchemba (kushoto) akimsikiliza Kaimu Mkurugenzi wa Mifumo ya
Kompyuta (TEHAMA) wa Mamlaka ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Mohamed
Khamis (wapili kushoto) alipokuwa akielezea jinsi wanavyosajili taarifa
mbalimbali za waombaji wa vitambulisho. Waziri Mwigulu alitembelea Kituo
hicho cha Usajili na kujifunza kazi mbalimbali zinazofanywa na NIDA,
jijini Dar es Salaam leo. Watatu kushoto ni Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa
Mamlaka hiyo, Andrew Massawe.
Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka
ya Vitambulisho vya Taifa (NIDA), Andrew Massawe (wapili kushoto-mbele)
akimsindikiza Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba (kushoto
mstari wa mbele) mara baada ya Waziri huyo kumaliza ziara yake ya
kutembelea ofisi za NIDA Makao Makuu na ofisi zake za usajili wa taarifa
mbalimbali za waombaji wa vitambulisho, zilizopo jijini Dar es Salaam.
0 maoni:
Chapisha Maoni