Jumamosi, 12 Novemba 2016

UBALOZI WA CHINA WAWAKUMBUKA WAANDISHI WA VITABU VYA ZAMANI: WILLIAM SHAKESPEARS NA TANG XIANZU

Posted by Esta Malibiche on NOV 12,2016 in NEWS

Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Mathew ya Jijini Dar es Salaam wakiangalia machapisho mbalimbali ya vitabu vilivyoandikwa na Waandishi wa zamani akiwemo Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza ikiwa ni sehemu wakati wa maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi hao wa vitabu vya zamani yaliyofanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Wanafunzi wa Shule ya Sekondari ya Mtakatifu Mathew ya Jijini Dar es Salaam, James Edward (kushoto) na mwenzake Abdulaziz Ahmed wakibadilishana mawazo na Mkufunzi wa somo la lugha ya kichina, Zhu Yajing wakati wa maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu na William Shakespeare. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Mkuu wa Idara ya Utamduni katika Ubalozi wa China nchini, Gao Wei akizungumza na wageni waalikwa katika maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Naibu Kaitbu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Millao akizungumza na wageni waalikwa katika maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing.
Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing akizungumza na wageni waalikwa katika maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Naibu Kaitbu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Millao.
Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing akimkabidhi zawadi Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Millao katika maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing akimpa maelezo ya ufafanuzi ya vazi la asili, Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Millao katika maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam.
Balozi wa China nchini, Dkt. Lu Youqing akisalimia na Ayubu Tewele, mwanafunzi wa mwaka wa pili wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam anayesoma soko la lugha ya kichina wakati wa maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam. Katikati ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Millao.
Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Bi. Nuru Millao akibadilishana mawazo na Maofisa Waandamizi wa Ubalozi wa China nchini, akiwemo Balozi Dkt. Lu Youqing (kulia) wakati wa maadhimisho ya miaka 400 ya kuwaenzi waaandishi wa vitabu vya zamani Tang Xianzu wa China na William Shakespeare wa nchini Uingereza. Maadhimisho hayo yalifanyika leo Jijini Dar es Salaam.

(PICHA NA MAELEZO).

……………………………………………………………..

Na Beatrice Lyimo-MAELEZO-Dar es Salaam.

NAIBU Katibu Mkuu Wizara ya Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Nuru Millao ametoa wito kwa vijana wa kitanzania kutumia fursa ya ushirikiano uliopo baina ya Tanzania na China katika taaluma za masomo ikiwemo kusoma na kujifunza lugha ya kichina ili kuharakisha shughuli za maendeleo nchini.

Aliyasema hay oleo Jijini Dar es salaam wakati wa sherehe za ufunguzi wa maadhimisho na maonesho ya utamaduni wa china yaliyolenga kuenzi mchango wa waandisi wa vitabu wa zamani William Shakespeare wa Uingereza na Tang Xianzu wa China.

Bibi Nuru alisema kuwa kwa sasa Nchi ya China ipo mbali kimaendeleo hivyo wanafunzi wa wakitanzania hawana budi kutumia fursa hiyo katika kujifunza masuala mbalimbali ikiwemo lugha ya kichina. mbalimbali.

Aidha, Bibi Nuru aliwaasa watanzania kuiga tamaduni zinazofanywa na watu wa wachina katika kuenzi kazi za waandishi mbalimbali wa mashairi, vitabu, tamthilia na maigizo ili kuweza kufaidika katika nyanya tofauti za maendeleo nchini.

“Tanzania itafaidika vizuri zaidi wa kuiga mifano chanya ya wenzetu kwa kuenzi kazi za waandishi wa vitabu mbalimbali nchini, kwa mfano Mwalimu Nyerere aliandika vitabu vilivyochochea maendeleo ya Taifa” alifafanua Bibi Nuru.

Kwa upande wake Balozi wa China Nchini, Dkt. Lu Youqing alisema China itaendeleza ushirikiano uliopo baina yao na Tanzania katika sekta mbalimbali ili kuweza kuleta manufaa baina ya wananchi wa pande zote mbili.

Balozi Youqing alisema, kumekuwa na ushirikiano mzuri baina ya Tanzania na China hasa katika sekta ya utamaduni ambapo kwa sasa takribani vyuo vikuu Vinne nchini China vinafundisha lugha ya Kiswahili.

Aidha Dkt. Youqing alisema shule sita za Sekondari nchini Tanzania zina programu ya kufundisha lugha ya kichina ikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es salaam, tawi la Mlimani na pamoja na Chuo Kikuu cha Dodoma.

Aidha Balozi Youqing alisema kuwa, nchi ya nchina imekuwa ikitafsiri vitabu vya lugha Kiswahili kwenda kwenye lugha ya kichina ambapo wameweza kutafsiri vitabu vya Mwalimu Nyerere vinavyowasaidia katika ujenzi wa Taifa lao.

Maonyesho hayo ni sehemu ya maadhimisho ya miaka 400 ya waandishi wa vitabu vya riwaya, tamthilia na filamu wakiwemo William Shakespeare wa Uingereza na Tang Xianzu wa China.

0 maoni:

Chapisha Maoni