Posted by Esta Malibiche on Nov 8,2016 in BIASHARA
Meneja wa Uendelezaji Masoko wa TBL,Malaki Sitaki akizungumza
Baadhi ya wajasiriamali waliomaliza mafunzo ya RDP wilayani Bagamoyo katika picha ya pamoja
Baadhi ya wajasiriamali waliomaliza mafunzo ya RDP wilayani Ilala katika picha ya pamoja
Wajasiriamali waliomaliza mafunzo ya RDP wilayani Bagamoyo wakifurahi katika hafla ya kuwapongeza hivi karibuni
…………………………………………………………………………….
-Idadi yao kubwa ni wanawake
Kampuni ya TBL inaendelea
kutekeleza mpango wa kutoa elimu ya ujasiriamali kwa wateja wanaouza
bidhaa zake kupitia mpango wa Retail Development Programme ulioanza
mwaka jana unaoenda sambamba na elimu ya Unywaji Kistaarabu.
Meneja
wa Uendelezaji Mauzo wa TBL,Bw. Malaki Sitaki, amesema kuwa kwa kipindi
cha muda mfupi yamepatikana mafanikio makubwa kutokana na mwitikio
mkubwa wa wanaohitaji kupatiwa mafunzo ambapo kwa kipindi cha miaka 2
tayari mafunzo yamewafikia wajasiriamali zaidi ya 2,500
kutoka karibu mikoa yote nchini na matarajio ya kampuni ni kuwafikishia
elimu zaidi ya wajasiriamali 20,000 hadi ifikapo mwaka 2019.
“Mwitikio wa wahitaji wa mafunzo haya ni mkubwa na kinachofurahisha idadi kubwa ya wajasiriamali wanaoshiriki mafunzo
haya ni Wanawake.Hii kwetu ni faraja kubwa kwa kuwa tunaamini
kuwaelimisha wanawake inakuwa umeelimisha jamii nzima na ni rahisi
kuleta maendeleo na mabadiko endelevu kama ilivyo lengo la mpango huu”.Alisema Malaki
Alisema thatmini ya awali ya mpango imebainisha kuwa mafunzo yanaendelea kuwanufaisha wasambazaji wa bidhaa za TBL ngazi ya chini (Retailer level) na asilimia kubwa ya waliopata mafunzo haya wanaendelea kuendesha biashara zao na kujipatia faida inayowawezesha kuboresha maisha yao na familia zao kwa kuzipatia lishe nzuri,watoto wao kupata huduma bora za kiafya na elimu .” Huu ndio mwelekeo wa uwekezaji wetu unaokwenda sambamba na kuleta mabadiliko kwenye jamii”.Alisema.
Mafunzo
ambayo yametolewa kupitia mpango huu aliyataja kuwa ni mbinu mbalimbali
za kufanya biashara kwa mafanikio,utunzaji wa mahesabu na kumbukumbu za
mauzo,matumizi mazuri ya fedha,mipango ya biashara,sheria na miongozo
ya biashara,huduma kwa wateja,elimu ya unywaji kistaarabu na utunzaji wa
mazingira.
“Suala
la Unywaji wa Kistaarabu na mazingira tumeliweka kwenye mafunzo haya
kwa ajili ya kuendeleza kampeni inayoendelea ya kuhakikisha jamii
inatumia vinywaji kama viburudisho badala ya kulewa na kuleta athari kwa
jamii ikiwemo kushindwa kushiriki katika shughuli za uzalishaji mali
ipasavyo.”Alisema Malaki.
Aliongeza
kuwa TBL inatekeleza maazimio yaliyofikiwa na watendaji Wakuu wa
makampuni yanayotengeneza vinywaji vyenye kilevi wakati wa kuadhimisha
siku ya unywaji wa kistaarabu hivi karibuni ambapo waliazimia kujenga
jamii zisizoathirika na ulevi katika maeneo yanapofanyia biashara na kusambaza bidhaa zake.
Malaki
alisema elimu ya Unywaji Kistaarabu itaendelea kutolewa katika jamii
kupitia njia mbalimbali mojawapo ikiwa ni kuunga mkono jitihada za
serikali kupitia Jeshi la Polisi kwa kusaidia katika kampeni za usalama
barabarani kwa kuhamasisha madereva kutotumia vinywaji vyenye kilevi
pindi waendeshapo vyombo vya moto.
Mwaka
huu TBL ilikuwa mstari wa mbele kufanikisha Wiki ya Nenda kwa usalama
barabarani ambapo ilishiriki katika uhamasishaji wa Usalama barabarani
pia ilitoa huduma ya zahanati inayotembea ya ‘Zahanati Mwendo’ kwa ajili
ya kupima afya za madereva na kutoa ushauri wa kiafya huduma ya aina
yake nchini ambayo imewawezesha madereva wengi kupimwa afya zao na
kupatiwa ushauri wa kitaalamu.
0 maoni:
Chapisha Maoni