Posted by Esta Malibiche on Nov 15,2016 in NEWS
Mkurugenzi Idara ya Mashariki ya
Kati, Balozi Abdallah Abas Kilima, ambaye pia ni mwanakamati wa kamati
ya Kuzuia na Kupambana na Biashara haramu ya Kusafirisha Binadamu nchini
akitoa maelezo kwa wageni kutoka Malawi namna Tanzania inavyopambana na
changamoto zinazotokana na kupinga na kuzia biashara haramu ya binadamu
. Wageni hao kutoka Malawi walitembelea ofisi za Wizara ya Mambo ya
Ndani ya Nchi kwa lengo la kujifunza hatua mbalimbali zinazochukuliwa
nchini na wadau ili kupambana na biashara hiyo haramu. ((Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Katibu wa Kamati ya Kuzuia
Usafirishaji Haramu wa Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi ,
Seperatus Fella akizungumza wakati wa kikao na wageni (hawako pichani)
kutoka nchini Malawi chini ya Kanisa la Misaada la Norway waliokuja
kujifunza hapa nchini ni namna gani Taifa na wadau mbalimbali
wanapambana na biashara haramu ya kusafirisha binadamu pamoja na Mpango
kazi wa mwaka ili kufikia malengo. Wa kwanza ni Mkurugenzi Idara ya
Mashariki ya Kati, Balozi Abdallah Abas Kilima, ambaye pia ni
mwanakamati wa kamati ya Kuzuia na Kupambana na Biashara haramu ya
Kusafirisha Binadamu. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Mkuu wa Programu wa Kanisa la
Misaada la Norway nchini Malawi Bi. Hayley Elizabeth Webster (katikati)
akiuliza swali kwa kamati ya Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu
hawapo pichani kwa namana gani serikali imejipanga kupambana na biashara
hiyo kwa kutoa elimu kwa jamii licha ya kuwa na bajeti finyu kama
ilivyo elezwa na mmoja wa wanakamati hao. Wengine ni wajumbe kutoka
kanisa hilo la Misaada nchini Malawi walioambatana nae ili kujifunza
namba ambavyo Tanzania imekua ikipambana na biashara hiyo. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Katibu wa Kamati ya Kuzuia
Usafirishaji Haramu wa Binadamu kutoka Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi,
Seperatus Fella (wa pili kulia), akizungumza wakati wa kikao na wageni
kutoka nchini Malawi chini ya Kanisa la Misaada la Norway waliokuja
kujifunza hapa nchini ni namna gani Taifa na wadau mbalimbali
wanapambana na biashara haramu ya kusafirisha binadamu pamoja na Mpango
kazi wa mwaka ili kufikia malengo. Wa kwanza ni Mkurugenzi Idara ya
Mashariki ya Kati, Balozi Abdallah Abas Kilima, ambaye pia ni
mwanakamati wa kamati ya Kuzuia na Kupambana na Biashara haramu ya
Kusafirisha Binadamu. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
Baadhi ya Wanakamati wa Kamati ya
Kuzuia Usafirishaji Haramu wa Binadamu na wajumbe kutoka nchini Malawi
chini ya Kanisa la Misaada la Norway wakiwa katika picha ya pamoja
baada ya kumaliza majadiliano yaliyofanyika katika ukumbi wa Wizara ya
Mambo ya Ndani ya Nchi juu ya namna Tanzania inavyopambana na Biashara
Haramu ya Usafirishaji Binadamu. (Picha na Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi)
0 maoni:
Chapisha Maoni