Zaidi
ya wasanii 300 wa filamu mkoani Mwanza, jana wakifuatilia mafunzo
kuhusu weledi wa sanaa ya filamu kutoka kwa mkufunzi, Richard Ndunguru,
wa Chuo Kikuu cha Dar es salaam.
Mafunzo
hayo ni ya siku tatu ambapo yameandaliwa bure na Bodi ya Filamu nchini,
yalianza juzi Novemba 10 na yatafikia tamati leo Novemba 12,2016 ambapo
washiriki watakabidhiwa vyeti na Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Wasanii,
waongozaji pamoja na waandishi wa filamu wamepatiwa mafunzo hayo ili
kuboresha kazi zao ikiwemo kuzingatia kazi zenye maadili na maudhui ya
mtanzania na zaidi kutambua haki zao ikiwemo hakimiliki za kazi zao na
namna ya kuuza kaziuza kwa faida.
Mkufunzi,
Richard Ndunguru, kutoka Chuo Kikuu cha Dar es salaam, akiwasilisha
mada jana kwenye mafunzo ya sanaa ya filamu mkoani Mwanza.
Washiriki wa mafunzo ya sanaa ya filamu mkoani Mwanza
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo hayo wameishukuru Serikali kupitia Bodi ya
Filamu nchini kwa kuwafikishia mafunzo hayo bure na kwamba yatawasaida
kuboresha kazi zao na kulifanya soko la filamu mkoani Mwanza kukua.
Bonyeza HAPA Kuhusu Mafanikio ya Mafunzo
0 maoni:
Chapisha Maoni