Jumatano, 16 Novemba 2016

MRATIBU WA SPANEST MKOA WA IRINGA GODWELL MEING'ATAKI AKABIDHI VIFAA VYA MICHEZO


Posted by Esta Malibiche on Nov 16,2016 in MICHEZO

MRATIBU wa mashindano ya SPANEST Cup 2016 Godwell Olle Meing’ataki amekabidhi vifaa vya michezo kwa timu nane  za mpira kati ya 22 zilizoingia robo fainali katika mashindano ya Spanest Cup.



Timu zilizopata nafasi ya kuingia robo Fainali ni pamoja na Kitisi , Nyamahana , makifu mapogoro,  Luganga , Itunundu ,Kinyika na Mbugani huku ligi hiyo ikiwa na na kauli mbiu ya “Piga Vita Ujangili Piga Mpira Okoa Tembo”.


Akikabidhi  vifaa kwa  timu   hizo,mratibu wa  mashindano hayo  alisema kuwa toka  kuanza kwa lingi  hiyo  wananchi  wamekuwa  wakipewa  elimu ya namna ya  kuwafichua  watu  wanaojihusisha na vitendo  vya ujangili na  kuwa  hadi  sasa  mbali ya  kuwepo kwa changamoto mbali mbali  ikiwemo ya  baadhi ya  timu kuonyesha nidham mbaya  wakati wa mechi  ila vijana wameonyesha  kiwango kikubwa uwanjani



Alizitaja  timu  zilizofanikiwa  kuingia hatua ya robo fainali na pointi  zake katika mabano    kwa  tarafa ya  Idodi  kuwa ni Kitisi (12), Nyamahana(6) , makifu (5)na mapogoro(12)  wakati  tarafa ya Pawaga ni  Luganga (14), Itunundu (12),Kinyika(16) na Mbugani (10).


Meng’ataki alisema  robo fainali ya  kwanza  itakuwa na  timu  za Nyamahana  itacheza na  timu ya Kitisi  kwenye uwanja wa Nyamahana    huku Makifu na Mapogolo zitacheza   uwanja wa Makifu Novemba 17 mwaka huu  ,  Luganga na Kinyika  zitacheza katika uwanja wa Luganga  na Itunundu  na Mbugani  zitacheza uwanja wa Itunundu  Novemba 18 mwaka huu .

‘’’’Katika  robo faina ya  pili ya ligi   hiyo ya Spanest Cup 2016  Novemba 19  timu ya  Kitisi itacheza  na Nyamahana  katika  uwanja wa Kitisi  na Mapogolo  itacheza na  Makifu  kwenye  uwanja wa Kinyika   wakati Novemba 20 itakuwa ni hitimisho ya robo fainali ya  pili kwa   timu ya  Kinyika  kucheza na Luganga kwenye uwanja wa Kinyika na  Mbugani na Itunundu  zitacheza  uwanja wa Mbugani  na  kuwa  mechi  zote  zitaanza kwa  wakati na  kila timu  kuhakikisha  saa 9 ;00 Alasiri inakuwepo uwanjani ikiwa  imevaa sare kabisa’’’’Alisema Meng’ataki .


Aidha aliongeza kuwa hatua ya  nusu fainali  itachezwa  Novemba 22 na fainali  itachezwa  Novemba 26  mwaka huu iwapo ratiba   hiyo haitavurugika  na fainali hiyo itachezwa tarafa ya Idodi .



‘’’’Mshindi wa kwanza atapata kikombe, medali ya dhahabu, seti moja ya jezi, cheti, Sh 300,000, kutembelea Hifadhi ya Ruaha.Mshindi wa pili atapata medali ya fedha, mipira 2, cheti na Sh 200,000 taslim huku mshindi wa Tatu akipata medali ya shaba, cheti na Sh 100,00 huku mshindi wa nne atazawadiwa  Sh 50,000’’’’Alisem,a Meng’ataki




Mratibu wa  mashindano ya SPANEST Cup 2016  Godwell Olle Meing’ataki (kulia)  akimkabidhi  vifaa vya  michezo  Kiongozi wa  timu ya  Itunundu Fc Eliopa Maurosi  na afisa mtendaji wa kijiji  cha Itunundu  Halima Kunzugala  wakati wa  zoezi la kugawa vifaa kwa  timu nane kati ya 22  zilizofuzu hatua ya  robo fainali ya  ligi ya Spanest  Cup 2016.

0 maoni:

Chapisha Maoni