Posted by Esta Malibiche on Nov. 30,2016 in NEWS
Matofali yaliyofyatuliwa na
wanafunzi Mradi wa Elimu ya Kujitegemea yanatumika kujengea vyoo na
madarasa pale penye upungufu wa vyumba vya madarasa na Vyoo (Picha na
Bizei)
Baadhi ya wanafunzi wakila chakula shuleni.
Matofali yaliyofyatuliwa na
wanafunzi Mradi wa Elimu ya Kujitegemea yanatumika kujengea vyoo na
madarasa pale penye upungufu wa vyumba vya madarasa na Vyoo (Picha na
Bizei)
……………………………………………………………………..
Judith Mhina – MAELEZO
Shule za Msingi za Serikali
katika Halmashauri ya Buhigwe zipo 88 zamuenzi Baba wa Taifa Mwalimu
Julius Nyerere kwa kutekeleza kwa vitendo miradi 102 ya Elimu ya
Kujitegemea.
Hayo yamesemwa na Waratibu Elimu
Kata 5 wa Halmashauri hiyo, waliokuwa wakihudhuria Mafunzo ya siku
mbili yaliyoendeshwa na Mpango wa Kuinua Elimu Tanzania EQUIP – TZ,
Mwezi Novemba mwaka huu, katika Ukumbi wa VanCity katika Halmashauri ya
Wilaya ya Kasulu Kigoma.
Kiongozi wa Waratibu Kata hao
Mwalimu Maxmillan Joseph alisema:” Halmashauri ya Buhigwe imefanikiwa
kwa kiasi kikubwa kuwa na miradi ya elimu ya kujitegemea na
kupunguza dhana ya utegemezi kwa serikali kwa asilimia mia moja”.
Mwalimu Maxmillan aliongeza :”
Mfano zoezi zima la utengenezaji wa madawati katika Mkoa wa Kigoma,
mbao zilizo nyingi zimetoka katika miradi ya kujitegemea ya Shule za
Msingi za Buhigwe, hili ni jambo la kujivunia.”
Miradi ya shule hizo za Msingi
ina lengo la kuwaandaa wahitimu katika shule hizo kujengewa uwezo wa
kujitegemea kuilingana na mazingira ya mahali walipo na kuanzisha
shughuli zao mara baada ya kuhitimu darasa la saba.
Aidha, baadhi ya miradi hiyo
inahusu shughuli za Kilimo, Ufugaji, Misitu, Mazingira, Ufyatuaji na
uchomaji matofali na biashara ya vifaa vya elimu Mfano shule ya Msingi
Mwayaya ipo Kata ya Mwayaya ina mradi wa duka la vifaa vya elimu vya
rejareja, Shule ya Gwimbogo kupanda miche ya mikaratusi robo ekari,
shule ya Kibila mradi wa migomba nusu ekari, Shule ya Manyovu ufugaji
wa kuku 30 na mbuzi 3 majike
Kata ya Muhinda shule ya Ruhuba A
robo ekari bustani ya mbogamboga Ruhuba B, kilimo cha Migomba nusu
ekari, shule ya Nyarubo ina mradi wa ufugaji mbuzi jike 1, shule
Muhinda kuku 10 wa asili, shule ya Kigaraga uboreshaji shamba la kahawa
ekari
nusu. Kata ya Buhigwe shule ya
Buhigwe mradi wa migomba robo hekari, shule ya Kavomo shamba la miti
robo ekari na shamba la mbegu za majani ya malisho ya wanyama robo
ekari. Shule ya Nyankoronko kilimo cha mahindi nusu ekari, shule ya
Mulera migomba nusu ekari, na mananasi robo ekari shule ya Nyamiti
kilimo cha mananasi nusu ekari, shule ya Kafene mananasi nusu ekari.
Shule Kavomo mbogamboga za
kupanga kwenye maji yaani saladi na mradi wa ng’ombe 2 majike wa maziwa
shule ya Rusaba upandaji mti 200 robo ekari Rusaba B upandaji miti ya
kahawa 200 robo ekari, shule ya Mpanzigo uendelezaji shamba la kahawa
nusu ekari. Nyarabingo upandaji wamiche ya kahawa 150 robo ekari. Shule
ya Kibwiga kilimo cha migomba ekari shule ya Kiyanga kilimo cha
mananasi, nusu ekari shule ya Mikanda duka la vifaa vya elimu Nyaregano
kuku wa mayai 100 shule ya Kilalama ufugaji wa kuku wa asili 40.
Pamoja na miradi yote hiyo ya
shule kiwango cha elimu cha Halmashauri ya Buhigwe kimepanda kutoka
nafasi ya 6 ya wilaya mpaka 4. Kama ifuatavyo, Mwaka 2013 ilikuwa
nafasi ya 6, 2014 ilikuwa 5, 2015 5 2016 4 ki Mkoa
Itakumbukwa Muasisi wa Taifa hili
Marehemu Mwalimu Julius Kambarage Nyerere na Azimio la Arusha ambalo
lilitoa muongozo wa Elimu ya Kujitegemea. Katika Awamu ya Mwalimu na
dhana ya kujitegemea ilianza kujengwa kwa mtoto kuanzia shule ya Msingi,
Sekondari, Vyuo vya Ufundi, Vyuo Vikuu na sehemu za kazi kila Afisa
au Mtumishi wa Serikali alitakiwa kuwa mfano katika kufanya mradi au
shghuli yoyote ya kujitegemea ili mradi isijihusishe na matumizi mabaya
ya fedha za umma au ya nafasi yako kazini.
Dhana hii ya Mwalimu Nyerere,
iliweza kujenga Taifa la watu wenye uwezo wa kumudu maisha yao ya kila
siku bila kufikiri kuna baba, mama, mjomba au shangazi wa kukuhudumia
kama kijana. Tafiti mbalimbali zinaonyesha Vijana wengi wa Tanzania
hawawezi kubuni, kutafakari muelekeo wa maisha yake binafsi na kupelekea
lawama zote kuiangukia Serikali kwamba haitoi ajira kwa vijana.
Pamoja na juhudi za Serikali ya
Awamu ya Tano ya kuandaa nafasi nyingi za uongozi kwa vijana na kuweka
mazingira mazuri kwa vijana kujiajiri, bado tatizo ni kubwa la vijana
kupenda kufanya shughuli ambazi sio endelevu na ambazo haziwezi
kuwajengea uimara wa kumudu maisha yao ya kila siku.
Wilaya ya Buhigwe ni mfano wa
kuigwa na Tanzania nzima kwani shule za Msingi 88 zote zinamiradi ya
kujitengemea, jambo la kusikitisha Mkoa wa Kigoma Halmashauri zote
zilizobakia hazina miradi ya elimu ya kujitegemea kama Buhigwe. Hakika
Buhigwe mnastahili pongezi , ushauri wangu ni vema mkahakikisha Mkoa wa
Kigoma wote unakuwa mfano bora kwa Watanzania kwani ardhi ipo yenye
rutuba haihitaji mbolea kutukana na asili yake ya udongo uliotokana na
Volkano na uwepo wa bonde la ufa la Ziwa Tanganyika. volkano
0 maoni:
Chapisha Maoni