Posted by Esta Malibiche on Nov 8,2016 in NEWS
Baadhi
ya wapanda boda boda kati ya 250 waliojiunga na Mfuko wa Pensheni wa
PPF kupitia mpango wa "Wote Scheme wilayani Temeke jijini Dar es Salaam,
wakionyesha mfano wa kadi za kujiunga na mpango huo baada ya
kukabidhiwa na Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva,
wakati wa uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoani Dar es Salaam,
Novemba 7, 2016.
Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Mkemwa William Faustin.
NA
K-VIS BLOG/KHALFAN SAID
MFUKO
wa Pensheni wa PPF umeendelea na kampeni yake ya kuandikisha wanachama wapya
kupitia mpango wa “Wote Scheme”, unaohusisha wafanyakazi walio katika sekta
rasmi na wale waliojiajiri wenyewe ambapo katika uzinduzi wa wiki ya nenda kwa
usalama mkoani Dar es Salaam, zaidi ya waendesha bodaboda 250, kutoka wilaya ya
Temeke, walijiunga na mpango huo.
Katika
uzinduzi huo uliofanyika viwanja vya Mwembe-Yanga, wilayani humo Novemba 7,
2016, Mkuu wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, ambaye alimwakilisha
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, aliwakabidhi kadi za uanachama wa
Mfuko huo baadhi ya waendesha bodaboda hao.
Akizungumza
baada ya zoezi hilo la kuwakabidhi kadi hizo, Meneja Uhusiano wa PPF, Bi. Lulu
Mengele alisema, zoezi la kuandikisha wanachama wapya wakiwemo hao wa bodaboda,
litakwenda sambamba na maadhimisho ya Wiki ya nenda kwa usalama ambayo
itafanyika kwenye wilaya za Ilala, na Kionondoni pia.
“Tunatoa
wito kwa, wananchi wote, wakiwemo wajasiriamali, mama lishe, bodaboda,
machinga, kujiunga na mpango huo ambao una faida nyingi ikiwemo kujipatia bima
ya afya, mikopo ya elimu na mafao mengine mengi.” Alifafanua.
Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Lowowa Emmanuel Julius
Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya uanachama wa PPF, mpanda bodaboda, Rubamande Ratifa Ally
Bw. Lyaviva, akimkabidhi mfano wa kadi ya PPF, Bw. Shinne Gustaph Patrick
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Jackson Lyaviva, akimpongeza mwanachama mpya wa PPF, ambaye ni dereva wa Bodaboda, Bw.
Mkemwa William Faustin
Mkemwa William Faustin
Mkuu
wa wilaya ya Temeke, Felix Jackson Lyaviva, akisalimiana na Kamanda wa
Polisi Kanda ya Temeke, Kamishna Msaidizi Mwandamizi wa Polisi, (SACP),
Gilles Mroto wakati akiwasili. Kulia ni Kamanda wa Polisi Kanda ya
Ilala, Salum Hamduni
Kamanda
wa polisi wa Kikosi cha Usalama Barabarani wilaya ya Temeke, Mrakibu
Msaidizi wa Polisi, (ASP), Solomon Mwangamilo, akizungumza jambo na
Meneja Uhusino wa PPF, Bi. Lulu Mengele. Kushoto ni Afisa Uhusiano wa
Shirika la Nyumba la Taifa, (NHC), Bw. Yahya Charahani
Mkuu wa wilaya ya Temeke, Felix Jackson Lyaviva, akisalimiana na Kamanda wa Polisi Kanda ya Ilala, Salum Hamduni
Mkuu
wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, akisalimiana na Kamanda
wa Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Wilaya ya Temeke, ASP, Solomon
Mwangamilo
Meneja
Uhusino wa PPF, Bi. Lulu Mengele, akisalimiana na Kamanda wa Kikosi cha
Usalama Barabarani wilaya ya Kinondoni, Kamishna Msaidizi wa Polisi,
(ACP_, Theopista Malya
Meneja
Uhusino wa PPF, Bi. Lulu Mengele, akisalimiana na Mkuu wa Kituo cha
Polisi, (OCS), cha Mabasi ya Mkoa, Ubungo Bus Terminal, Mrakibu Msaidizi
wa Polisi, (ASP), Sarah Bundala
Polisi wa usalama barabarani wakiingia kwa maandamano kwenye viwanja vya Mwembe-Yanga
Askari
wa usalama barabarani akiyaelekeza magari yaliyoshiriki kwenye
maanadamano siku ya uzinduzi wa wiki ya nenda kwa usalama mkoa wa Dar es
Salaam, viwanja vya Mwembe-Yanga
Waendesha Bodaboda wakiwasili kwa maandamano kwenye viwanja hivyo
Mwanachama
mpya wa PPF, ambaye ni mwendesha bodaboda, Ratifa Ally, (kushoto),
akibadilishana mawazo na Maafisa wa PPF Kanda ya Temeke, Elizabeth
Chambiri, (kulia) na Donald Maeda
Brass Band ya polisi ikiongoza maandamano |
Mkuu
wa wilaya ya Temeke, Bw. Felix Jackson Lyaviva, (kulia), akipatiwa
malezo ya shughuli za Mfuko wa Pensehni wa PPF, kutoka kwa Msimamizi wa
Kanda ya Temeke, Sospeter Lyimo, (wapili kushoto). Kulia ni Bi.
Elizabeth Chambiri
Afisa
Uhusiano Mwandamizi wa PPF, Bi. Jannet Ezekiel, akimpatia maelezo Afisa
huyu wa polisi kuhusu mpango wa Wote Scheme, ambao Polisi nao wanaweza
kujiunga nao
Mwanachama mpya akisajiliwa kujiunga na Wote Scheme
0 maoni:
Chapisha Maoni