Ijumaa, 11 Novemba 2016

UZINDUZI WA MAJENGO YA WODI ZA KINAMAMA NA WATOTO HOSPITALI YA MNAZI MMOJA

Posted by Esta Malibiche on NOV 12,2016 in NEWS

1
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akimkabidhi zawadi Bw.Trond Mohn kutoka Nchini Norway ambaye kati ya wadhili waliotoa fedha kwa Ujenzi  majengo mapya ya Wodi za Kinamama na Watoto ambayo yamefunguliwa leo katika Hospitali ya Mnazi Mmoja Mjini Unguja majengo hayo yamejengwa kwa ufadhili kutoka Nchini Uholanzi,Norway na kushirikiana Serikali ya Mapinduzi
2
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein na Mkewe Mama Mwanamwema Shein (katikati) wakipata maelezo wakati walipotembelea moja ya Chumba cha Xray katika majengo mapya ya Wodi za Kinamama na Watoto wakati alipotembelea baada ya ufunguzi rasmi wa majengo hayo uliofanyika leo,ambayo yamejengwa kwa ufadhili kuoka Nchini, Uholanzi,Norway na kushirikiana Serikali ya Mapinduzi
3
Vitanda vya kisasa vilivyomo katika moja ya Wodi ya Kinamama katika majengo mapya  zikiwemo na wodi za Watoto  yaliyofunguliwa leo na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,ambapo yamejengwa kwa ufadhili kutoka nchini Norway,Uholanzi na kushirikiana na Serikali ya Mapinduzi,
4
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akipata maelezo kutoka kwa Muuguzi katika majengo mapya ya Wodi za Kinamama na Watoto Jogha Abdalla Ali wakati alipotembelea baada ya ufunguzi rasmi wa majengo hayo uliofanyika leo,ambapo yamejengwa kwa ufadhili wa Uholanzi,Norway na kushirikiana Serikali ya Mapinduzi.
5
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein,akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Teresia  Mcha (kulia) katika sherehe ya ufunguzi wa majengo mapya ya Wodi za Kinamama na Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja zilizofanyika leo,majengo hayo yaliyojengwa kwa ufadhili wa Serikali ya Uholanzi na Norway,(kushoto) Mtendaji Mkuu wa Hospitali ya Chuo Kikuu cha Hauklend Bw.Eivend Hansen.
6
Mke wa Rais wa Zanzibar Mama Mwanamwema Shein akipokea zawadi kutoka kwa Mwakilishi wa Ubalozi wa Uholanzi Teresia  Mcha (kulias) katika sherehe ya ufunguzi wa majengo mapya ya Wodi za Kinamama na Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja zilizofanyika leo,mgeni rasmi akiwa Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein
7
Mawaziri wa Wizara mbali mbali pamoja na Wananchi waliohudhuria katika sherehe ya Ufunguzi wa Majengo mapya ya Wodi za Kinamama na Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipokuwa akitoa hutuba yake leo baada ya ufunguzi rasmi wa majengo hayo.
8
Madaktari kutoka Nchi mbali mbali wanaotoa huduma kwa wananchi wa Zanzibar wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) wakati alipokuwa akitoa hutuba yake leo katika sherehe ya Ufunguzi wa Majengo mapya ya Wodi za Kinamama na Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja,baada ya ufunguzi rasmi wa majengo hayo.
9
baadhi ya Wafanyakazi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja wakimsikiliza Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein (hayupo pichani) alipokuwa akitoa hutuba yake leo katika sherehe ya Ufunguzi wa Majengo mapya ya Wodi za Kinamama na Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja,baada ya ufunguzi rasmi wa majengo hayo,yaliyojenga kwa ufadhili kutoka Nchini Uholanzi,Norway na kushirikiana Serikali ya Mapinduzi
10
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akizungumza na wananchi katika ufunguzi wa majengo mapya ya Wodi ya Kinamama na Watoto katika Hospitali ya Mnazi Mmoja ambayo yamefadhiliwa na Uholanzi na Norway sherehe za ufunguzi zimefanyika,
[Picha na Ikulu.] 11/11/2016.

0 maoni:

Chapisha Maoni