Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Mashaka Gambo (aliyesimama) akiongea na madereva wa boda boda kuwaelezea
mpango wa Serikali wa kuwapatia Pikipiki 200.
Baadhi ya waendesha boda boda wakifuatilia kikao kilichoitishwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha
Kaimu Katibu Tawala wa Wilaya Ndg.
Polycarp Nkuyumba(aliyesimama) akiwakaribisha viongozi na wadau kwenye
Kikao na waendesha boda boda wa Wilaya ya Arusha.
Lucas Malusu ni dereva wa boda boda
Kutoka Kata ya Elerai (aliyesimama katikati) akitoa maoni yake katika
kikao chao na Mkuu wa Mkoa wa Arusha.
Serafini Shirima(aliyesimama) ni dereva
wa boda boda kutoka Kata ya Levolosi akichangia uanzishwaji wa umoja wa
wandesha boda boda Wilaya ya Arusha (UBOJA)
Viongozi wa mpito waliochanguliwa
kusimamia taratibu za uanzishjwaji wa Umoja huo pamoja na utoaji wa
Pikipiki wa vijana nane wa Kila Kata.
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho Gambo
(aliyesimama mbele) akihitimisha kikao chake na waendesha boda boda wa
Wilaya ya Arusha.
Nteghenjwa Hosseah
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Mrisho
Mashaka Gambo amekutana na waendesha bodaboda wa Jiji la Arusha na
kuwajulisha kuhusu mpango wa Serikali wa kuwakwamua kiuchumi kwa
kuwawezesha kupata Pikipiki bila Riba wala dhamana.
Rc Gambo amekuja na Mpango huu wa Kuinua
uchumi wa Vijana kwa kuwapatia Pikipiki baada ya kukutana na kundi hili
la waendesha boda boda kwa mara na kusikiliza malalamiko yao huku
miongoni mwa kero yao kubwa ni kutozwa fedha nyingi na wamiliki wa boda
boda hizo.
Akiongea na waendesha boda boda Rc Gambo
alisema ninaona jinsi mnavyojituma katika kujitafutia riziki lakini
hamthaminiki na kazi hii imekua ikidharaulika, sasa muda umefika kwa
kazi hii kuwa ya heshima mbele ya Jamii, kila kijana aliyepo katika
biashara hii ataweza kumiliki Pikipiki yake na sio kuendesha Pikipiki za
watu ambao wamekuwa wakiwanyonya kila siku kwa kuwatoza Fedha nyingi na
wao kuzidi kuneemeka wakati ninyi mnazidi kuwa masikini.
“Kundi hili limekuwa likitumiwa kwa
maslahi ya watu wachache kwa kuwa wamekuwa wakipewa Pikipiki hizo kwa
faidi kubwa na mmiliki anapokea Fedha zaidi yya mara mbili ya bei ya
kununulia Pikipiki hiyo ndipo aamue kummilikisha kijana pikipiki hiyo au
aamue kuendelea kupokea Fedha kwa kipindi chote wakati ninyi mnapata
tabu barabarani huko na mnaambulia Fedha kidogo kiasi ambacho hamuwezi
fikia hatua ya kumiliki Pikipiki zenu” Alisema Gambo.
Aliongeza kuwa Serikali ya Mkoa wa Arusha
imeona ni vyema ikawajengea uwezo vijana waliopo katika kazi hii kwa
kuwapa mafunzo na kuwapatia Pikipiki ambazo mtatakiwa kurejesha kiasi
cha Fedha halali iliyonunuliwa Pikipiki hiyo kisha kumilikishwa chombo
bila ya riba yeyote wala dhamana.
Aliendelea kusema utoaji wa Pikipiki hizi
utazingatia Kata zote zilizopo katika Jiji la Arusha ili Pikipiki
ziweze kuwafikia walengwa na zoezi hili litaendelea kwa vijana wengine
kadiri ya mahitaji; Tutaongeza usimamizi kwa wote watakaopata Pikipiki
hizi ili waweze kurejesha Fedha kama inavyotakiwa na tuweze
kuwanunulia vijana wengine hatimaye tuwafikie vijana wote wenye uhitaji
wa kumiliki na kufanya biashara ya bodaboda.
Serafini Shirima ni dereva wa boda boda
Kata ya Levolosi akizungumza katika Kikao hicho alisema kwa mara ya
kwanza Katika Mkoa huu wamepata mlezi anayetambua na kuthamini kazi ya
boda boda na aliyethubutu kuwatafutia Pikipiki za bei nafuu ili kuongeza
kipato cha vijana wa Arusha.
Shirima alishauri kuundwa kwa kamati ya
mpito itakayosimamia na kuratibu mchakato mzima wa vijana watakaoanza
kupewa Pikipiki hizo na kukamilisha taratibu zote za uanzishaji wa umoja
wa wandesha Boda boda utakaofahamika kwa jina la (UBOJA) chini ya Mlezi
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. Gambo.
RC Gambo alikamilisha Kikao hicho kwa
kusimamia uchaguzi wa viongozi wa mpito kutoka katika Kila Kata na
hatimaye kupatikana viongozi watano watakaoratibu mpango wa awali wa
utoaji wa Pikipiki kwa vijana.
Pikipiki zitakazotolewa katika awamu ya
kwanza ni 200 zikiwa na thamani ya Tsh Mil 400 na zitatolewa sanjari na
Bima kubwa(Comprehensive Insurance) kwa vijana 200 ambapo kila Kata
itatakiwa kutoa vijana 8.
Vijana wa Arusha watakabidhiwa Pikipiki
hizi na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassimu
Majaliwa tarehe 03/12/2016 kwenye uwanja wa Sheikh Amri Abeid
0 maoni:
Chapisha Maoni