Posted byEsta Malibiche on Nov 16,2016 in MICHEZO
Na Luteni Selemani Semunyu
JAJI
Mkuu wa Tanzania Mh Othman Chande anatarajiwa kuwa Mgeni rasmi katika
mashindano ya gofu ya Mkuu wa Majeshi mstaafu Generali Geogre Waitara
maarufu Waitara Trophy 2016.
Hayo
yamesemwa na Mwenyekiti wa Klabu ya Golf ya Jeshi la ulinzi la wananchi
wa Tanzania ya Lugalo wanaoandaa mashindano hayo Brigedia Jenerali
Michael Luwongo wakati akizungumza na waandishi wa habari Jijini Dar Es
salaam.
Brigedia
Jenerali Luwongo alisema maandalizi yamekamilika na yanatarajiwa
kufanyika Jumamosi Novemba 19 na kushirikisha Wachezaji wa makundi yote
isipokuwa watoto huku klabu zote zikithibitisha kushiriki.
“Tumeshajiandaa
vya kutosha na wadhamini wametuwezesha na mwitikio mpaka sasa ni mkubwa
na tayari wachezaji 150 wametibitisha kushiriki mashindano haya
yanayodhaminiwa na kampuni ya Serengeti kupitia kinywaji chake cha John
Walker red label” Alisema Generali Luwongo.
Aliongeza
kuwa mbali na Vilabu wenyeji klabu ya Lugalo ,Gymkhana Dar es
Salaam,Gymkhana Morogoro ,Gymkhana Arusha, Kili,na TPC Moshi ,na Mufindi
pia kutoka Arusha Mkuu wa majeshi Mstaafu Mirisho Sarakikya
amethibitisha kushiriki katika mashindano hayo.
Pia
alisema Wanatarajia kuongea na Chama cha Golf Nchini ili kuona namna
gani baadhi ya Mashindano ya Ndani ikiwemo hili la Waitara kuwa na hadhi
ya Kimataifa kutokana na kuwa mashindano hayo na hamasa kubwa iliyopo.
Kwa upande wake Nahodha wa Klabu ya Lugalo Kapten Japhet Masai alisema mashindano
hayo yatakuwa ya Stroke play Net ambapo yatatanguliwa na Wachezaji wa
Kulipwa na Wachezaji wasaidizi siku ya Ijumaa Novemba 18 huku siku
inayofuata yakifanyika kwa makundi yaliyosalia.
Naye
Meneja wa mawasiliano wa Serengeti Abbas Abraham alisema maandalizi ya
zawadi ikiwemo ya Vikombe yamekamilika na wanachosubiri ni zoezi la
kukabidhiwa kwa Washindi.
Mashindano ya Kombe la Waitara yanayofanyika kila mwaka ikiwa
ni kumbukumbu ya kutambua mchango mkubwa uliotolewa na mkuu huyo wa
majeshi katika kuanzisha Uwanja wa Golf wa Lugalo Mwaka 2006.
0 maoni:
Chapisha Maoni