Posted by Esta Malibiche on NOV 30,2016 In NEWS
Kiwango
cha ufaulu wa mitihani ya kumaliza elimu ya msingi Mkoani Singida
kimepanda kutoka wastani wa asilimia 58.41 mpaka asilimia 69.25 ikiwa ni
ongezeko la asilimia 11 huku wanafunzi 14,759 wakichaguliwa kujiunga na
masomo ya sekondari kwa kidato cha kwanza kwa mwaka 2017.
Buhacha
Baltazar Kichinda akiongoza kikao cha uteuzi wa wanafunzi wa kidato cha
kwanza kwa mwaka 2017 kama Kaimu Katibu Tawala Mkoa na mwenyekiti wa
kikao hicho amesema mkoa umefaulisha wavulana 6,852 na wasichana7,907
huku akiwapongeza waalimu wote kwa bidii ya ufundishaji iliyopelekea
mkoa wa singida kushika nafasi ya 12 kati ya Mikao 26 ya tanzania bara.
Kichinda
ameipongeza halmashauri ya Itigi kwa kushika nafasi ya kwanza kati ya
halmasahuri saba za mkoa wa singida na ya 38 kitaifa kati ya halmashauri
186 za Tanzania bara huku ikifaulisha kwa asilimia 80.41. Aidha
amewatia moyo halmasahuri ya Mkalama kwa ufaulu hafifu wa 57.51 na kuwa
nafasi ya 155 kitaifa.
Kichinda
ameongeza kuwa kwa sasa kila Mkurugenzi wa halmasahuri anapaswa kukaa na
wadau wake wa elimu ili kupanga mikakati ya kuboresha zaidi elimu,
amesema lengo kubwa kwa sasa ni kuhakikisha kila mwanafunzi aliyefaulu
anajiunga na kidato cha kwanza na kumaliza elimu ya sekondari.
Amesema
sekta ya elimu inachangamoto mbalimbali ikiwemo utoro wa walimu na
wananfunzi, miundombinu ya vyumba vya madarasa kutotosheleza mahitaji
halisi, upungufu wa waalimu, uhaba wa nyumba za walimu pamoja na waalimu
wenyewe kuwa wachache tofauti na mahitaji halisi hivyo amewata wadau wa
elimu kujipanga kutatua changamoto hizo na sio kusubiria serikali kuu
kufanya kila kitu.
Aidha
kichinda amesema kuwepo na utaratibu wa kuwapongeza waalimu hasa kwenye
shule zilizofanya vizuri ili iwe motisha kwa kazi wanayoifanya huku
akiitangaza shule ya msingi Utaho ya halmasahuri ya Ikungi kuwa ya
kwanza kimkoa kwa shule zenye wananfunzi zaidi ya 40 na shule ya msingi
Aghondi ya Itigi kuwa ya kwanza kimkoa kwa shule ambazo zina wanafunzi
chini ya 40.
Naye Mkuu
wa Wilaya ya Singida Elias Tarimo amesema ili kuboresha elimu mkoani
Singida msisitizo uwepo wa kuhakikisha wananfunzi wote wanapata chakula
shuleni ili waweze kusikiliza kwa umakini mzuri.
Tarimo
ameongeza kuwa wazazi wanapaswa kutambua kuwa elimu bila malipo
haiwaondolei wajibu wao kama wazazi wa kuhakikisha wanafunzi wanakula,
wanalala na kuvaa hivyo hivyo watakaposhirikishwa katika kuchangia
chakula, ujenzi wa mabweni au shuguli za elimu wajitoe kwani wamiliki wa
shule ni wazazi.
Amesema
utaratibu wa kufanya ukaguzi ili kuwatambua waalimu watoro au wazembe
ufanyike katika halmashauri zote na kwa viongozi wote wanaotembelea
vijijini bila ya kusubiri ziara maalumu ya ukaguzi na kuongeza kuwa hali
hiyo itawaongezea umakini waalimu katika kutekeleza majukumu yao lakini
pia watendaji watabaini changamoto za waalimu na shule na kuzitatua kwa
uharaka.
0 maoni:
Chapisha Maoni