Posted by Esta Malibiche on Nov 29,2016 in NEWS
UMOJA
wa Ulaya (EU) na Umoja wa Mataifa (UN) wamejiunga pamoja kuendesha
kampeni ya uelewa wa malengo ya maendeleo endelevu (SDGs) nchini
Tanzania . Aidha kwa pamoja wamezuru miradi iliyofadhiliwa na EU. Wakiwa
Mkoani Iringa wamepata nafasi ya kuzungumza na wanachuo 1,000 kutoka
vyuo vikuu vya Iringa na Mkwawa kwenye semina iliyoelezea malengo hayo
ya dunia ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani.
Kampeni hiyo imelenga kuwafanya vijana waelewe malengo 17 ya dunia
ambayo kwa sasa yana mwaka mmoja tangu yapitishwe na kuwatanabaisha
wajibu wao katika kufanikisha utekelezaji wake ndani ya mazingira ya
Tanzania.
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro
(kushoto) akisalimiana na mmoja wa wahadhiri wa chuo hicho alipowasili
katika ofisi za Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua
Madumulla akiwa ameambatana na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP), Alvaro Rodriguez.
Semina
katika vyuo hivyo ni sehemu ya mpango madhubuti wa Umoja wa mataifa
uliozinduliwa Arusha Mei mwaka huu na Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa, Bw. Alvaro Rodriguez wenye lengo la kuwaelimisha vijana zaidi
ya 30,000 ifikapo mwaka ujao kuhusu malengo hayo ya dunia. Ujumbe huo wa
EU na UN pia ulipata nafasi ya kutembelea miradi mbalimbali
inayofadhiliwa na EU ukiwamo wa Boma la Kijerumani ambalo lilikarabatiwa
kwa ruzuku ya EU kupitia ‘fahari yetu – Southern Highlands Culture
Solutions’. Boma hilo ni moja ya majengo ya zamani katika mji wa Iringa
na lilijengwa na Wajerumani mwaka 1900 kama hospitali ya kijeshi. Baada
ya vita ya Kwanza ya Dunia, jengo hilo lilibadilishwa matumizi na
watawala wapya, Uingereza, na kulifanya kuwa jengo la utawala. EU
imesema inaona fahari kuwa mmoja wa wawekezaji wakubwa katika sekta ya
sanaa na urithi wa kitamaduni nchini Tanzania, ikifadhili miradi 10
iliyo chini ya programu ya 10 ya EDF ya kusaidia masuala ya kitamaduni.
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla akiwa kwenye
mazungumzo na Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini
ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (upande wa kushoto katikati)
pamoja na Mtaalam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa Tanzania, Hoyce
Temu (kushoto) alipotembelewa ofisini kwake na ugeni huo. Kulia ni
Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever pamoja na Katibu Tawala
Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa Iringa, Henry Mditi.
Masuala
yanayohusu urithi wa kitamaduni ni muhimu katika kuchagiza ukuaji wa
uchumi, ajira na huku ikifuma mahusiano ya kijamii, na kutoa fursa ya
kuboresha utalii endelevu mkoani Iringa huku ikileta faida kwa wakazi wa
eneo hilo. Bw. Rodriguez, akizungumza katika kampeni hiyo alisema
kwamba ajenda 2030 ambayo ni ajenda ya maendeleo endelevu inahitaji
ushiriki wa kila mmoja.Aliwapongeza wanachuo hao na wanazuoni kwa
kujikita kutambua malengo hayo ya dunia. Aidha aligusia umuhimu wa
vijana kushiriki katika masuala ya maendeleo kutokana na ukweli kuwa,
kwa taifa kama la Tanzania vijana ni asilimia 60 ya wananchi wote
waliopo.Alisema kwamba vijana wanajukumu kubwa la kushiriki katika
maendeleo hayo kwa lengo la kuipeleka nchi katika hatua
nyingine ya maendeleo.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwa
ameongozana na Katibu Tawala Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa Iringa,
Henry Mditi kuelekea kwenye ukumbi wa mikutano Chuo Kikuu cha Iringa.
Hata
hivyo alisema kwamba ni wajibu wa kila mtu hasa vijana, kuhakikisha
kwamba malengo hayo ya dunia yanafanikiwa . Alisema Umoja wa Mataifa kwa
kusaidiwa na wadau wake muhimu kama Umoja wa Ulaya, utaendelea kusaidia
Watanzania kuwajibika katika shughuli mbalimbali za maendeleo katika
kuunga mkono malengo hayo ya dunia. Mmoja wa washiriki alipongeza Umoja
na wa Mataifa kwa kuwafikia vijana wa vyuoni na kuwapa semina hiyo.
“Ninajisikia mtu mwenye bahati kupata nafasi ya kujifunza maendeleo
endelevu kutoka kwa Mratibu wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini.
Nikiwa kama kijana, naona faraja kuona kwamba viongozi wetu wanafuata
maelekezo yaliyofafanuliwa kwenye malengo 17 ya maendeleo endelevu;
naamini kama tukijitahidi kuyafikia ifikapo 2030, basi Tanzania na
duniani kwa ujumla itakuwa eneo jema la kuishi. Na kwa kuwa sasa
natambua kuhusu malengo hayo ya dunia, ninaweza kutoa mchango wangu
kusaidia kuyafikia -najisikia kuwezeshwa sana.” amesema Mary, mmoja wa
washiriki.
Mkuu
wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla akisoma taarifa
fupi ya Chuo Kikuu cha Iringa mbele ya ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa na
Umoja wa Ulaya wakati semina kuhusu malengo ya Maendeleo Endelevu
(SDGs) ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani kwa
wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.
Mkuu
wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akizungumza kwenye semina ya
malengo ya dunia kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa ambapo aliwaasa
wakawe mabalozi wazuri wa malengo hayo kwenye jamii zao na wanafunzi
wenzao wa vyuo vingine.
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro
akitoa salamu za Umoja wa Ulaya kwa niaba ya Balozi wa Umoja huo, Bw.
Roeland Van De Geer wakati wa semina Malengo ya Maendeleo Endelevu
(SDGs) kwa wanachuo wa Iringa iliyowezeshwa na EU.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akiwapiga
msasa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa kuhusu Malengo ya Dunia katika
semina iliyofadhiliwa na Umoja wa Ulaya (EU) mjini Iringa.
Mwanafunzi
wa mwaka wa tatu anayechukua Shahada ya Sayansi katika Uchumi na Fedha
wa Chuo Kikuu cha Iringa, Sarafina Sayi akiuliza swali kwa mkufunzi wa
malengo ya dunia Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini
na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez (hayupo pichani) wakati wa semina hiyo.
Mwanafunzi
wa Shahada ya Sayansi katika Uchumi na Fedha wa Chuo Kikuu cha Iringa,
Geoffrey Kadori akiuliza swali kwa Mkuu wa Wilaya ya Iringa, Richard
Kasesela wakati wa semina ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) ambayo
ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu duniani kwa wanafunzi wa
Chuo hicho.
Mkuu
wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela akijibu swali wakati wa kipindi
cha maswali na majibu kwenye semina kuhusu malengo ya maendeleo endelevu
(SDGs) kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.
Pichani
juu na chini ni wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa kutoka vitivo
tofauti chuoni hapo waliohudhuria semina ya malengo ya Maendeleo
Endelevu (SDGs) ambayo ni sehemu ya ajenda 2030 ya maendeleo endelevu
duniani kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa iliyofadhiliwa na Umoja
wa Ulaya (EU).
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi
Mkuu wa Chuo Kikuu cha Iringa (UOI), Prof Joshua Madumulla makabrasha na
majarida yenye ripoti na taarifa mbalimbali za Umoja wa Mataifa.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akimkabidhi
Mkuu wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela ripoti na makabrasha
mbalimbali ya Umoja wa Mataifa mara baada ya kuhitimisha semina kuhusu
SGDs kwa wanafunzi wa Chuo Kikuu cha Iringa.
Mkuu
wa wilaya ya Iringa, Richard Kasesela (wa tatu kulia) katika picha ya
pamoja na ujumbe kutoka Umoja wa Mataifa, Umoja wa Ulaya pamoja na
Balozi wa Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs Champion), Sabinus Paul
(kushoto) nje ya ukumbi kulikofanyika semina kuhusu SDGs kwa wanachuo wa
Iringa.
Picha ya pamoja na sehemu ya washiriki wa semina hiyo huku wakiwa na mabango ya SDGs.
Muonekano
wa nje wa jengo la Makumbusho ya Mkoa na Kituo cha Utamaduni -Iringa
Boma ambalo limejengwa kwa ufadhili wa Umoja wa Ulaya (EU).
Kibao cha Makumbusho ya Mkoa wa Iringa kinachoratibiwa na Mradi wa Fahari yetu kwa kushirikiana na Chuo Kikuu cha Iringa
Meneja
wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever akielezea dhumuni la mradi Fahari
Yetu unaolenga kuendeleza utamaduni nyanda za juu kusini kwa Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez (wa pili
kushoto) aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini
ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro (mwenye suti) ambao ndio wafadhili
wa jengo hilo la Makumbusho ya Mkoa wa Iringa. Wengine katika picha ni
wahadhiri na maprofesa kutoka Chuo Kikuu cha Iringa.
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akisaini
kitabu cha wangeni ndani ya Makumbusho ya mkoa wa Iringa.
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro
akisaini kitabu cha wageni alipowasili katika Makumbusho ya mkoa wa
Iringa.
Meneja
wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever akitoa maelezo picha mbalimbali
zinazoelezea historia ya mkoa wa Iringa wakati wa utawala wa Chifu
Mkwawa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini
ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro walipotembelea makumbusho ya mkoa
wa Iringa
Mratibu
Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika
la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro Rodriguez akisoma
historia mbalimbali za enzi za utawala wa kichifu ndani ya Makumbusho ya
Mkoa wa Iringa.
Mwongoza
wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Jacob Shenyagwa (mwenye
miwani) akitoa maelezo ya picha mbalimbali kwa ugeni huo wa UN na EU
uliotembelea makumbusho hiyo iliyojengwa chini ya ufadhili wa Umoja wa
Ulaya (EU).
Mwongoza
wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Deonis Mgumba akitoa
maelezo ya vifaa mbalimbali vilivyokuwa vikitumika enzi za utawala wa
kichifu kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa Mataifa nchini na
Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa (UNDP), Alvaro
Rodriguez (kushoto) na Katibu Tawala Msaidizi -Miundombinu wa Mkoa wa
Iringa, Henry Mditi (katikati) walipotembelea makumbusho hayo mjini
Iringa.
Mwongoza
wageni katika Makumbusho ya mkoa wa Iringa, Matatizo Kastamu akitoa
maelezo ya picha mbalimbali zenye kumbukumbu za utawala wa kichifu na
historia ya mji wa Iringa kwa Mratibu Mkazi wa Mashirika ya Umoja wa
Mataifa nchini na Mwakilishi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa
(UNDP), Alvaro Rodriguez aliyeambatana na Mwakilishi wa Umoja wa Ulaya
(EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro.
Mwakilishi
wa Umoja wa Ulaya (EU) nchini ambaye pia ni Afisa Miradi, Anna Muro
(kushoto), Mtalaam wa Mawasiliano wa Umoja wa Mataifa nchini, Hoyce Temu
na Meneja wa Mradi wa Fahari Yetu, Jan Kuever wakipitia vipeperushi
vyenye maelezo ya kina ya Mradi wa Fahari Yetu unaoendesha Makumbusho na
Kituo cha Utamaduni mkoa wa Iringa.
0 maoni:
Chapisha Maoni