Jumanne, 8 Novemba 2016

HALMASHAURI YA IRINGA YAIDHINISHA KUTUMIKA KWA SHERIA ZA VIJIJI



 Posted by Esta Malibiche on Nov 8,2016 in NEWS


Na Esta Malibiche
Iringa

HALMASHAURI ya Wilaya ya Iringa imeidhinisha kuanza kutumika kwasheria ndogo  ya usimamizi wa maliasili (misitu na wanyamapori) ilikukabiliana na kasi ya uharibifu wa rasilimali za mistu na wanyamapori katika vjijini husika.

Sheria iliyoidhinishwa na Halmashauri hiyo imetungwa na Halmashauri za vijiji vya Mbweleli,Kinyika na Kinyali chini ya msaada wa Chama cha Wanasheria Watetezi wa Mazingira LEAT  lengo likiwa kudhibiti uharibifu wamazingira unaokuwa kwa kasi katika maeneo ya vijijini.

Akizungumza mara baada ya baraza la madiwani   la Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuidhinisha kuanza kutumika kwa sheria hizo katika kikoa cha baraza hilo kilichoketi  juzi, mwenyekiti wa halmashauri hiyo Stephen  Mhapa alisema sheria hizo zitasaidia kuongezaa kasi ya utunzaji wa mazingira na wanyamapori katika vijiji husika.

Alisema Halmashauri za vijiji zinamamlaka kamili ya kutunga sheria ndogo zinazohusu usimamizi wa maeneo yao na kwamba sheria hizo zisipingne na sheria mama za nchi na Halmashauri husika.

“Kitendo cha halmashauri za vijiji kutunga sheria ndogo ya kusimamia kudhibiti uharibifu wa mazingira katikia eneo lao kimenifurahisha na kwamba kuanzia sasa mistu na wanyama waliokuwa katika hatari ya kutoweka kutokana na uwindaji na uchomaji moto vitakuwa salama”alisema Mhapa na kuonmgeza:

“Hiyo ni kutokana na wananchi wa eneo husika wao wenyewe kwa hiyari yao kujitungia sheria wanazoweza kuzisimamia ,katika hili niwashukuru Chama cha Wanasheri Watetezi wa Mazingira (Leat)ambao wamewapatia elimu na msaada wa kufikia hatua hiyo ya kutunga sheria ndogo watakazoweza kuzisimamia wao wenyewe”alisema.

Mwanasheria mkuu wa Halmashauriu hiyo Kissah Mbilla alisema jukumu la ofisi yake katika mchakato huo pamoja na kushirikiana na wanasheria wa LEAT ilikuwa kuhakikisha sheria hiyo ndogo hazipingana nasheria mama ambayo ni ileya Halmashauri nay a Nchi.

“Halmashauri ya kijiji inayo mamlaka ya kutunga sheria ndogo na ofisi yetu inachofanya ni kuangalia kama taratibu zimefuatwa,adhabu zinazotolewa katika sheria hizo ndogo za kijiji zisizidi Sh 50,000 na kwakuiwa wamepitisha na baraza la madiwani limeidhinisha hizi sasa ni sheria kamili na zinaweza kuanza kutumika”alisemaMbilla.

Kwa upande wake Mkuu wa Idara ya Ardhi na Maliasili wa Halmashauari hiyo Donald Msham alisema kuidhinisha wa kwa sheria hizo kutasaidia idara yake kupambana na uharibifu wa mazingira ambao kwa sasa umekuwa ukishika kasi.

Alisema hatua hiyo inawez akuwa ya mafanikio kutokana na sheria hizo tangu mchakato w akutunga hadi kuidhinishwa na barazaz la madiwani umeshirikisha wananchi katika kufikia malengo hayo.

Afisa habari wa chama cha wanasheria watetezi wa mazingira (Leat) Edina Tibaijuka alisema hatua ya baraza la madiwani kuidhinisha kutumika kwa sheria hizo kumewafariji kwakuwa jukumu lao la kuelimisha wananchi na kuwahamasisha kutunga sheria hizo linakuwa limetimia.

Edina alisema Leat waliamua kutekeelza mradi huo w akuwasaidia wanavijiji kutunga sheria baada ya kupitia na kuona sheria walizokuwa wakizitumia awali zinamapungufu.

“Baada ya mkutano wa mkuu wa kijiji kuridhia na kupitisha sheria hiyo ya mazingira Leat wamezichapisha na kitendo cha baraza lamadiwani kuridhiakuanza kutumika kunatoa fuirsa kwa serikali za vijijikuanza kutumia sheriahizo kudhibiti vitendo vya uharibifu wa mazingira”alisema.Tibaijuka.

0 maoni:

Chapisha Maoni