Posted by Esta Malibiche on Nov 17,2016 in BIASHARA
Mkurugenzi
wa Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji Yuda Thadeus Mboya
(katikati) akizungumza wakati wa ufunguzi wa semina ya wajasiriamali
iliyoandaliwa na Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania (Tanzania Private
Sector Foundation),(Kulia) Meneja wa SIDO mkoa Kigoma, Gervas Ntahamba
na (wa pili kushoto) Mwenyekiti wa chama cha Wafanyabiashara na wenye
viwanda mkoa Kigoma (TCCIA), Ramadhani Gange.
Mwenyekiti
wa chama cha Wafanyabiashara na wenye viwanda mkoa Kigoma (TCCIA),
Ramadhani Gange (wa pili kushoto aliyesimama) akitoa neno la shukrani
kwa mgeni Rasmi wakati wa ufunguzi wa semina kwa wajasiliamali
iliyotayarishwa na taasisi ya sekta binafasi Tanzania (TPSF) .
Baadhi
ya wajasiliamali wa Manispaa ya Kigoma Ujiji wakijadiliana mada
mbalimbali zilizotolewa na wawezeshaji wakati wa semina ya wajasiriamali
iliyoandaliwa na taasisi ya sekta binafasi Tanzania (TPSF).
Wajasiriamali
waliopo mkoani Kigoma wametakiwa kutumia raslimali mbalimbali zilizopo
mkoani humo na fursa zinazojitokeza kwa sasa kuibua miradi ya biashara
na kuendesha biashara yao kitaalamu wakiwa na malengo ya kujikwamua
kutoka katika hali ya umaskini. Ushauri huo umetolewa na Mkurugenzi wa
Halmashauri ya Manispaa ya Kigoma Ujiji , Yuda Thadeus Mboya, wakati wa
ufunguzi wa mafunzo maalumu ya mbinu za kuendeleza wajasiriamali
yaliyoandaliwa na taasisi ya Tanzania Private Sector Foundation (TPSF)
na kufanyika katika ukumbi wa St.Martha mjini Kigoma.
Alisema
serikali imefungua milango ya kuwasaidia wafanyabiashara wadogo kwa
kutumia fursa zilizopo hivyo aliwataka kushiriki mafunzo mbalimbali ya
mbinu za biashara na kuibua miradi ya biashara na kuwa na utayari wa
kukabiliana na changamoto mbalimbali zilizopo katika biashara kwa
kipindi hiki mojawapo ikiwa ni ushindani mkubwa na kufanya biashara kwa
kufuata njia halali zinazotakiwa ikiwemo kulipa kodi za serikali kwa
mujibu wa sheria.
Hivi
sasa biashara zinafanyika katika mazingira ya ushindani na wateja
wanahitaji bidhaa zenye ubora hivyo haitakiwi ubabaishaji wa aina yoyote
kwa mfanyabiashara anayetaka mafanikio”.Alisema Mboya. Aliipongeza
taasisi ya TPSF kwa kuendesha miradi ya mafunzo kwa wajasiariamali
sehemu mbalimbali nchini “Nawapongeza kwa kuwafikishia mafunzo
wajasiriamali wa ngazi za chini katika ngazi ya mikoa na wilaya kwa kuwa
wafanyabiashara wakipata mafunzo kama haya kwa vyovyote wataweza kupata
mafanikio katika shughuli zao”.Alisema .
Kwa
upande wake Meneja Mradi wa Mafunzo kutoka taasisi ya TPSF,Celestine
Mkama alisema kuwa taasisi hiyo inaendesha mradi wa kuwapatia mafunzo
wajasiriamali kuhusiana na mbinu mbalimbali za kufanya biashara kwa
lengo la kupata mafanikio.
“Mafunzo
haya yamelenga kuwapatia maarifa wafanyabiashara wadogo ili yawajengee
uwezo wa kukabiliana na changamoto zilizopo katika biashara “Tafiti
nyingi zinaonyesha kuwa wafanyabiashara wengi wadogo wamekuwa wakikosa
mbinu za kufanya biashara kutokana na kukosa elimu ya biashara ndio
maana tumeona tuwasaidie katika eneo hili la kuwajengea uwezo kupitia
kuwapatia elimu ya ujasiriamali”.Alisema Bw.Mkama.
Mkama
alisema baadhi ya masuala yanayofundishwa kupitia mafunzo haya ni
utunzaji wa mahesabu ya biashara,nidhamu katika matumizi ya
fedha,utunzaji wa kumbukumbu za biashara na jinsi ya kupanga miradi.
Alisema mafunzo haya tayari yameishafanyika katika mikoa mbalimbali na
kuwafikia wajasiriamali wengi na tathmini ya awali inaonyesha kuwa
waliopata mafunzo haya wameanza kuendesha biashara zao kwa ufanisi na
kutoa mchango katika pato la taifa kupitia kulipa kodi.
0 maoni:
Chapisha Maoni