Jumamosi, 12 Novemba 2016

MKUU WA MKOA WA ARUSHA MRISHO GAMBO AZINDUA DARAJA LA ENGOTOTO

Posted by Esta  Malibiche on Nov 12,2016 in NEWS

Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akizindua daraja la Engototo lililofadhiliwa na Bw Hans Paul Jijini Arusha lililogharimu  zaidi 65Mill.

Daraja la Engototo lilozinduliwa na Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo
 Katika uzinduzi huo wananchi walimshukuru Mkuu huyo wa Mkoa kutokana na adha kubwa waliyokuwa wakiipata kutokana na ukosefu wa Daraja imara.
Wananchi walimlilia mkuu wa Mkoa huyo,kuhusu changamoto inayowakabili ya ukosefu wa Zahanati.


 Mkuu wa mkoa akizungumza mara baada ya kuzindua Daraja hilo,na kuwaahidi wananchi kuwapelekea bati 100,  Hans Pope akaahidi kutoa tofali 5000 na  Jagjit Aggarwal akaahidi kutoa mifuko 200 ya Cement kwa ajili ya ujenzi wa Zahanati hiyo
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mrisho Gambo akivishwa vazi Rasmi la kimira kutoka kwa wazee,alipowatembelea na kuzindua Daraja la Engototo

0 maoni:

Chapisha Maoni