Posted by Esta Malibiche on Nov 28,2016 in NEWS
Dampo la kisasa lilojengwa katika eneo la Chidaye Manispaa ya Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua ujenzi la
Dampo la kisasa lililopo eneo la Chidaye nje kidogo ya manispaa ya
Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akipata maelezo
kutoka kwa Mkurugenzi wa Manispaa ya Dodoma, Godwin Kunambi kuhusu
ujenzi wa Dampo la kisasa eneo la Chidaye.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua ujenzi wa
barabara ya lami ya Sango katika eneo la Soko kuu la majengo, Manispaa
ya Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akipokea maelezo ya
ujenzi wa barabara ya lami ya Sango katika eneo la Soko kuu la majengo,
Manispaa ya Dodoma.
Naibu Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo akikagua ujenzi wa
barabara ya lami ya Sango katika eneo la Soko kuu la majengo, Manispaa
ya Dodoma.
…………………………………….
NAIBU Waziri Ofisi ya Rais, Tawala za
Mikoa na Serikali za Mitaa(Tamisemi), Selemani Jafo amefanya ziara
katika manispaa ya Dodoma huku akipiga marufuku wafanyabiashara kupanga
bidhaa zao kwenye barabara na kuwataka wafanye biashara zao kwenye
masoko au maeneo rasmi yaliyotengwa na Manispaa hiyo.
Akizungumza leo mara baada ya kukagua
ujenzi wa barabara ya Sango iliyopo katika soko kuu la majengo na ujenzi
wa dampo la kisasa,Jafo amesema serikali inawekeza fedha nyingi kwenye
barabara lakini mwisho wa siku barabara haionekani kutokana na watu
kupanga bidhaa zao.
Naibu Waziri huyo amesema kupangwa kwa
bidhaa za nyanya au vitunguu barabarani kumekuwa kukichafua barabara na
wakati mwingine kusababisha zisipitike kiurahisi na watumiaji wengine.
Ameagiza Manispaa hiyo kuhakikisha
malengo ya barabara hiyo yanafuatwa na kuwazuia wafanyabiashara hao ili
barabara hizo zitunzwe ziweze kudumu na kufikia malengo.
“Hivi karibuni nilitembelea barabara
hii na ilikuwa ni mbaya na ni eneo la kibiashara niliagiza Manispaa
kuhakikisha barabara hii inajengwa, nimefarijika sasa agizo
limetekelezwa,”amesema Jafo
Hata hivyo amesema kwa kuwa vikao
vimeanza vya kupendekeza Dodoma iwe jiji ni lazima ibaki maana yake na
thamani ya jiji ipatikane kwa watu kuweka bidhaa zao kwenye masoko
yanayotakiwa.
Kuhusu Dampo la kisasa lililopo eneo
la Chidaye mjini Dodoma, Jafo ameitaka manispaa kuhakikisha eneo hilo
halivamiwi na watu kwa kuwa kumekuwepo na tabia ya wananchi kuvamia
maeneo yanayojengwa miundombinu.
Naye, Mkurugenzi wa Manispaa ya
Dodoma, Godwin Kunambi amemuahidi Jafo kuwa atasimamia sheria ndogo
ndogo za manispaa kuhakikisha wafanyabishara wanafanya biashara zao
kwenye maeneo yaliyopangwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni