Posted by Esta Malibiche on Nov.17,2016 in NEWS
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akikata utepe
kuashiria kuzindua pamoja na kukabidhi Jengo la Maabara la Skuli ya
Sekondari ya Kitope aliloligharamia yeye pamoja na ufadhili wa Ubalozi
China Nchini Tanzania na Kampuni ya simu za mkononi yaTigo.
Mwalimu
wa Masomo ya Sayansi wa skuli ya Sekondari Kitope Mwalimu Ali Mohamed
aliyeshika kifaa cha Maabara akimuelezea Balozi Seif urahisi wa kazi
yao ya ufundishaji kwa sasa baada ya kupata Maabara yenye kukidhi
kiwango kinachokubalika kwa skuli za Sekondari.
Mwalimu
Ali Mohamed akiendelea kutoa maelezo kwa Balozi Seif jinsi wanafunzi
wa masomo ya sayansi katika skuli yao walivyofarajika kutokana na
kujengewa maabara iliyokamilika kwa kazi zao za vitendo.
Mwalimu
Wanu Ndende Juma akiwasilisha Risala ya walimu na wanafunzi wa skuli ya
Sekondari ya Kistope kwenye hafla ya uzinduzi na kukabidhiwa rasmi
jengo la Maabara ya skuli hiyo lililomalizika kujengwa pamoja na kuwekwa
vifaa vyake.
Baadhi
ya Wanafunzi wa skuli ya sekondari ya Kitope wakifuatilia matukio mbali
mbali yaliyojiri kwenye uzinduzi wa maabara ya skuli yao.
Mkuu
wa Wilaya ya Kaskazini “B” Ndugu Issa Juma akitoa salamu katika hafla
ya uzinduzi wa jengo jipya la maabara ya skuli ya sekondari ya kitope.
Waziri
wa Elimu Mh. Riziki Pemba Juma akimshukuru Mwakilishi wa Jimbo la
Mahonda Balozi Seif kwa uzalendo wake wa kuunga mkono sekta ya Elimu
wakati wa hafla ya uzinduzi wa Maabara ya skuli ya Kitope.
Picha na – OMPR – ZNZ.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi aliitahadharisha Jamii
kuelewa kwamba maendeleo kwa wana Taaluma wa Fani ya Sayansi iwe
Maskulini au vyuoni yataendelea kuwa ndoto iwapo hakutakuwa na mipango
imara ya kuimarisha miundombinu kwenye Majengo ya Maabara katika
maeneo husika.
Alisema
Wazazi kwa kushirikiana na Kamati za Maskuli na vyuo kupitia usimamizi
wa Wizara inayosimamia masuala ya Elimu bado wana jukumu la kuhakikisha
vilio vya Wanafunzi kutokana na kukabiliwa na ukosefu wa Maabara kwenye
Taasisi zao vinamalizika.
Balozi
Seif Ali Iddi ambae pia ni Mwakilishi wa Jimbo la Mahonda alitoa
tahadhari hiyo wakati wa hafla fupi ya kukabidhi pamoja na kulizindua
rasmi Jengo la Maabara ya Skuli ya Sekondari ya Kitope iliyomo ndani ya
Wilaya ya Kaskazini “B”.
Jengo
hilo aliloligharamia yeye pamoja na kupata msaada wa nguvu za ufadhili
wa baadhi ya vifaa kutoka Ubalozi wa Jamuhuri ya Watu wa China na
Kampuni ya mitandao ya simu za mkononi ya Tigo limegharimu jumla ya
shilingi za Kitanzania Milioni 38,780,000/-.
Balozi
Seif alisema wanafunzi wa Skuli ya Sekondari ya Kitope kwa sasa hawana
sababu ya kufanya vibaya katika mitihani yao ya Kitaifa kutokana na
kumalizika kwa Jengo hilo la Maabara ambalo lilikuwa kilio kwao na
walimu wao kwa karibu miaka Kumi sasa.
Aliwaasa
Wanafunzi hao kuhakikisha kwamba Vifaa walivyopatiwa kwenye Maabara ya
Skuli yao wataendelea kuvitunza kwa tahadhari ili viweze kudumu kwa
kipindi kirefu na kutumiwa pia na wanafunzi wenzao watakaofuatia baada
ya wao.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif aliupongeza na kuushukuru
Uongozi wa Ubalozi wa Jamuhuri ya Watu wa China hapa Nchini pamoja na
ule wa Kampuni ya Mitandao ya Simu za mkononi wa Tigo kwa upendo wao wa
kuunga mkono Sekta ya Elimu hapa Zanzibar.
Othman Khamis Ame
Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar
17/11/2016.
0 maoni:
Chapisha Maoni