Posted by Esta Malibiche on Nov 12,2016 in NEWS
Mkurugenzi
Mtendaji wa (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba (kulia), akimwongoza
Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa na
ujumbe wake kutembelea maeneo mbalimbali katika Kituo cha Ilala, jijini
Dar es Salaam, wakati wa ziara yake.
Mkurugenzi
Mtendaji wa (TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba (kulia) akimweleza
jambo Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa
(katikati) na Wataalam alifuatana nao katika ziara hiyo, wakati
alipotembeleaMradi wa Kuboresha Huduma ya Umeme katikati ya Jiji la Dar
es Salaam.
Baadhi ya mitambo iliyofungwa katika kituo cha Dar es Salaam City Center.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa (wa kwanza
kulia) akimsikiliza Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania
(TANESCO), Mhandisi Felchesmi Mramba (katikati) wakati alipotembelea
Mradi wa Kituo cha Kuboresha Miundombinu ya Umeme cha Ilala, jijini Dar
es Saalam. Wa kwanza kushoto ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati
na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana Pallangyo.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa (wa pili
kulia), akimsikiliza Mtaalam kutoka TANESCO, Gibson Abdallah (wa kwanza
kulia) alipokuwa akieleza namna mifumo ya umeme katika Kituo cha Ilala
inavyofanya kazi. Wa kwanza kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa(TANESCO),
Mhandisi Felchesmi Mramba anayefuata ni Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya
Nishati na Madini anayeshughulikia Nishati, Dkt. Mhandisi Juliana
Pallangyo. Wengine wanaofuatilia ni Wataalam kutoka Wizara ya Nishati na
Madini na TANESCO.
Mafundi wakiendelea na kazi za ujenzi wa miundombinu ya umeme Kusambza umeme katika Kituo cha Ilala jijini Dar Dar es Salaam.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa na ujumbe
aliofuatana nao, wakisikiliza maelezo ya kuhusu namna kituo cha
Kudhibiti Mifumo wa Usambazaji Umeme cha Mikocheni, kinavyofanya kazi.
Kaimu
Meneja wa Mradi wa Uboreshaji wa Miundombinu Katikati ya Jiji la Dare s
Salaam, Mhandisi Iddy Rashid (katikati) akimweleza Katibu Mkuu wa Wizara
ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa (wa kwanza kulia) na ujumbe
aliofuatana nao namna mifumo katika Kituo cha Dar es Salaam City Center
inavyofanya kazi.
Katibu
Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Prof. Justin Ntalikwa leo amefanya
ziara ya kutembelea Miradi mbalimbali ya Kuboresha Miundombinu ya
Usambazaji umeme jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuangalia maendeleo
ya utekelezaji wa miradi hiyo inayotekelezwa katika maeneo mbalimbali
jijini Dar es Salaam kupitia Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO).
Miongoni
mwa miradi aliyoitembelea ni Kituo cha Usambazaji Umeme Ilala
kinachojengwa chini ya ufadhili wa Shirika la Maendeleo la Japan (JICA),
Mradi wa Kuboresha Huduma ya Umeme Katikati ya Jiji la Dar es Saalam
katika Kituo cha Dar es Salaam City Centre na Mradi wa Kituo cha
Kudhibiti Mifumo ya Usambazaji umeme, kilichopo eneo la Mikocheni Jijini
Dar es Salaam.
Mara
baada ya kutembelea miradi hiyo, Prof. Ntalikwa amesema kuwa, kukamilika
kwake kutaimarisha miundombinu ya usambazaji umeme Jijini Dar es Saalam
na hivyo kuwezesha Jiji la Dar es Salaam kupata umeme wa uhakika.
Akizungumzia
kituo cha Kudhibiti Mifumo wa Usambazaji Umeme cha Mikocheni,
kilichojengwa na Serikali ya Finland na Tanzania ameeleza kuwa, kituo
hicho kimefungwa mashine za kisasa zinazotumia teknolojia za hali ya juu
kama zinazotumiwa katika nchi zilizoendelea na hivyo, kukamilika kwake
kutawezesha kuondoa tatizo la kukatika kwa umeme jijini Dar es Salaam
ikiwemo kubaini kwa haraka na moja kwa moja eneo lolote lenye hitilafu
kupitia mitambo hiyo na hivyo kuwezesha tatizo kushughulikiwa kwa
haraka.
“ Kwa
ujumla nimeridhishwa na kasi ya utekelezaji wa miradi ya kuboresha
miundombinu ya umeme inayotekelezwa jijini Dar es Salaam. Mradi wa
Kuboresha Huduma ya Umeme Katikati ya Jiji la Dar es Saalam, unatarajiwa
kuzinduliwa tarehe 16 Novemba,2016 na Mhe. Rais Dkt.John Magufuli.
Kukamilika kwake kutakuwa na manufaa makubwa kwa upatikanaji umeme
jijini Dar es Salaam,” ameongeza Prof. Ntalikwa.
0 maoni:
Chapisha Maoni