Ujumbe
kutoka kutoka jimbo la Eastern Cape kutoka nchini Afrika ya Kusini uko
nchini kwa ajili ya kujifunza kutoka Tanzania namna bora ya fursa za
kiuchumi kwa wanawake nchini, uwezeshaji wa wanawake na uendeshaji wa
Benki ya Wanawake Nchini.
Akiongea
na Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na
Watoto Bi. Sihaba Nkinga kiongozi wa Msafara wa ujumbe toka Afrika
Kusini Mbunge wa Jimbo la Eastern Cape, Mhe. Nancy Sihiwaji amesema
ziara yaoa inatokana na utekelezaji wa maazimio ya mkutano wa Wanawake
Afrika uliofanyika Nchini Afrika ya Kusini kuhusu uwezeshaji wanawake
kiuchumi.
Aidha
ujumbe huu umetambelea Wizara hii ili kujifunza na kupata uzoefu kutoka
Nchini ni kuona ni jinsi gani Tanzania kwa kushirikiana na Wizara ya
Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto wameweza kuanzisha na
kufungua Benki inayolenga kuwainua wanawake kiuchumi.
Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Njinsia, Wazee na Watoto
akiongea na wajumbe wa ujumbe wa jimbo la Eastern Cape hawapo pichani
kutoka Afrika Kusini leo ofisini kwake.
Mhe.
Nancy Sihiwaji Mbunge wa Jimbo la Eastern Cape akiteta jambo na Katibu
Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi.
Sihaba Nkinga alipomtembelea Wizarani kwake kwa leo katika ziara ya
mafunzo ya siku moja kupata uzoefu wa uwezeshaji wanawake kiuchumi hapa
nchini.
Mhe.
Nancy Sihiwaji Mbunge wa Jimbo la Eastern Cape na ujumbe wake pamoja na
Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Bi. Sihaba Nkinga wote katikati wakiwa katika picha ya pamoja leo
walipomtembelea kwa ziara ya mafunzo ya siku moja kupata uzoefu wa
uwezeshaji wanawake kiuchumi hapa nchini.
Mhe.
Nancy Sihiwaji Mbunge wa Jimbo la Eastern Cape akimkabidhi Katibu Mkuu
Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Bi. Sihaba
Nkinga zawadi ya skafu yenye ujumbe kutoka Jimbo la Eastern Cape leo
ofisini kwake jijini Dar es Salaam kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi
Idara ya Jinsia kutoka Wizara hiyo Bw. Timoth Mgonja.(PICHA ZOTE NA
ANTHONY ISHENGOMA)
0 maoni:
Chapisha Maoni