Jumapili, 20 Novemba 2016

WAZIRI WA UTAMADUNI NA SANAA WA AFRIKA YA KUSINI ATEMBELEA KITUO CHA MAENDELEO DAKAWA NA MAKABURI YA WAPIGANIA UHURU WA CHAMA CHA ANC MKOANI MOROGORO.

Posted by Esta Malibiche on Nov 20,2016 in NEWS

Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akizungumza na viongozi wa Kituo cha Maendelo Dakawa (hawapo pichani) wakati Waziri huyo na ujumbe wake walipotembelea kituo hicho na kujionea makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC.

Kaimu Mkurugenzi kituo cha Maendeleo Dakawa Bw. Elasto Nywage(kulia) akitoa maelezo ya kituo hicho kwa Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa wakati Waziri huyo na ujumbe wako walipotembelea kituo hicho na kujionea makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC.




Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa(katikati) akiangalia makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC yaliyopo Dakawa wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Kaimu Mkurugenzi kituo cha Maendeleo Dakawa Bw. Elasto Nywage(kulia) akimuonesha Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa(katikati) moja ya kaburi la wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC yaliyopo Dakawa wilayani Kilosa mkoani Morogoro.


Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa akiweka shada la maua katika eneo maalum katika makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC yaliyopo Dakawa wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Eneo la makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC yaliyopo Dakawa wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Kaimu Mkurugenzi kituo cha Maendeleo Dakawa Bw. Elasto Nywage(kulia) akimuonesha Waziri wa Utamaduni na Sanaa wa Afrika ya Kusini Mhe. Nathi Mthethwa(katikati) bango linaloelezea kuwa eneo hilo ndipo yalipo makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC katika wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

Bango linaloelezea kuwa eneo hilo ndipo yalipo makaburi ya wapigania Uhuru wa Afrika ya Kusini kutoka Chama cha ANC yaliypo wilayani Kilosa mkoani Morogoro.

0 maoni:

Chapisha Maoni