Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt.
Hamisi Kigwangalla, akiwa ameongzana na timu ya Serikali yenye wataalamu
na wanausalama wameendesha operesheni kali ya kusaka viroba feki na
pombe nyingine haramu katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam na
kufanikiwa kukama sehena kubwa ya bidhaa hizo feki na haramu kwenye
maeneo hayo.
Katika
operesheni hiyo, pia wamefanikiwa kukibaini kiwanda bubu
kinachotengeneza kinywaji aina ya konyagi na Smirnoff feki maeneo ya
Sinza Jijini Dar es Salaam. Kiwanda hicho kinatengeneza vinywaji hivyo
kwa kutumia ‘spirit’ ambayo inachanganywa na ‘gongo’; spirit, gongo,
chupa tupu na zilizojazwa, vizibo, vifungashio vimekamatwa.
Kwa
hatua hiyo Jeshi la Polisi inawashikilia watu wawili ambao inasemekana
wanafanya kazi pamoja na bwana Yusuf Abdul Kalambo, ambaye anatafutwa na
polisi mpaka sasa kwa tuhuma za kuendesha shughuli hizo.
Tazama Picha hapa chini wakati wa zoezi hilo:
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt.
Hamisi Kigwangalla akikagua bidhaa za feki akiwa pamoja na maafisa
wengine katika zoezi hilo eneo la Sinza.
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt.
Hamisi Kigwangalla akikagua bidhaa za feki akiwa pamoja na maafisa
wengine katika zoezi hilo eneo la Sinza
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt.
Hamisi Kigwangalla akiwa ameshika vifuniko vya bidhaa za pombe feki
katika moja ya kiwanda bubu cha kutengeneza pombe hizo aina ya Konyagi.
katika zoezi hilo eneo la Sinza
Naibu
Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe. Dkt.
Hamisi Kigwangalla akikagua bidhaa za feki akiwa pamoja na maafisa
wengine katika zoezi hilo eneo la Sinza.
0 maoni:
Chapisha Maoni