Posted by Esta Malibiche on Nov 17,2016 in NEWS
Mmoja wa Simba akiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi
Baadhi ya Mamba wakiwa wamepumzika katika hifadhi ya Taifa ya Katavi
Hawa ni Punda milia wakiwa katika Hifadhi ya Taifa ya Katavi
Kama kibao kinavyo onekana hili ni Eneo la Tambiko ambapo watu huja kusali na kutoa sadaka mbalimbali
Simba akiwa na mzoga wa Kiboko
Twiga akiwa katika hifadhi ya Taifa ya Katavi
Na Walter Mguluchuma wa Katavi yetu Blog
Hifadhi
ya Taifa ya Katavi inapatikana kusini Magharibi mwa Tanzania karibu na
Ziwa Tanganyika katika Wilaya za Mpanda ,Tanganyika na Mlele Mkoa wa
Katavi inapatikana katika latitude 6.63.7.34 kusini na na longitude
3.74.31.84 Mashariki.
Hifadhi
hii ilitangazwa kuwa Hifadhi ya Taifa mwaka 1974 ikiwa na ukubwa wa
kilometa za mraba 2253 iliongezwa ukubwa mwaka 1996 na kufikia ukubwa wa
kilometa za mraba 4471 na kuifanya kuwa Hifadhi ya tatu kwa ukubwa
Tanzania baada ya Ruaha na Serengeti .
Ilipata
jina lake kutokana na mzimu wa kabila la Wabende aliyejulikana kwa
jina la Katabi ambapo mpaka leo watu mbalimbali wamekuwa wakifika ndani
ya Hifadhi ya Katavi na kwenda kwenye mti ulioko kwenye Ziwa Katavi
wakiamini kuwa mzimu Katabi alikuwa akiishi hapo zamani kabla ya kuwepo
Hifadhi ya Taifa ya Katavi .
Jina
la Hifadhi hii lilijulikana kama Katabi kutokana na imani ya jamii hizo
kwa mzimu Katabi inaaminika kwamba mzimu Katabi una uwezo wa kufanya
miujiza ikiwemo kufanya mvua inyeshe , kuzuia magonjwa ya mlipuko kama
vile ndui na kutatua shida za watu mbalimbali .
Hifadhi
hii inafikika mwaka mzima kwa kupitia Mikoa ya Dares,salaam,Mwanza ,
Kigoma Arusha hadi Mpanda kupitia Tabora kwa kutumia usafiri wa ndege za
kukodi Chartered planes au kwa njia ya barabara kwa kupitia Mbeya na
Sumbawanga pia kwa kutumia usafiri wa Treni kutokea Tabora .
Katavi
'National Park' inawanyama wengi na adimu na wakubwa kuliko wanyama
wanaopatikana kwenye Hifadhi nyingine hapa Nchini kutoka na hari ya uoto
wa asili uliopo kwenye Hifadhi hii ambayo kwa sasa imeanza kupata
watalii tofauti na hapo awali .
Mbali
ya kuwepo kwa wanyama wengi madhari yake ni pana kuanzia uwanda
tambarare wa nyasi katika mkondo wa bonde la ufa hadi kwenye miteremko
mikali ambayo ni matawi mawili sambamba na bonde la ufa la Mashariki
maarufu kama bonde la ufa la Rukwa .
Uoto
uliopo unavutia unavutia sana kuanzia kuanzia Misitu iliyofunga mpaka
misitu ya wazi ,vichaka uwanda wa nyasi maziwa ya msimu ya Chada na
Katavi mabwawa na uoto kando ya mito .Wakati
wa kipindi cha mvua kuna aina nyingi za maua aina ya 'species'
mbalimbali za miti na majani aina za 'species' 226 za miti zimeisha
tambuliwa zikiwemo aina tatu zenye mvuto wa kisayansi .
Uhai
wa Hifadhi ya Katavi unategemea mto Katuma ambao humwaga maji yake ziwa
Katavi upande wa kaskazini ,Ziwa Chada na mbuga yenye eneo la kilometa
za mraba 425 ambayo hutuamisha maji Floodplain katikati ya Hifadhi ziwa
Chada hupokea pia maji kutoka mto Kapapa ambao mkondo wake hutokea
Kaskazini mwa Hifadhi ya Taifa Katavi .
Kuna
aina mbalimbali za wanyama pori ,idadi kubwa ya vipepeo na ndege wa aina
mbalimbali katika Hifadhi ya Katavi ni kivutio vikubwa kwa wageni idadi
ya watalii na shughuli za maendeleo ndani ya Hifadhi bado ni ndogo
hivyo kufanya mazingira kuwa asilia zaidi .
Baadhi
ya wanyama wanaopatikana kwenye Hifadhi ya Katavi ni makundi makubwa ya
Tembo , Nyati, Simba , Pundamilia , Mbwa mwitu , kongoni Swala pala ,
Nyemela na wanyama wengineo .Pia
kwenye eneo la mto Stalike na Iku utakuta kuna makundi makubwa sana ya
viboko na mamba ambapo kumekuwa na mapigano ya mara kwa mara na kufanya
eneo hilo kuwa kivutio kikubwa kwa watalii.
Upande
wa Hotel hifadhi hiyo inayo hotel nzuri za kufikia wagani ndani ya
Hifadhi iiingawa bado ni chache pia hotel nyingine zinapatikana katika
Kijiji cha Stalike ambacho kipo jirani na Hifadhi na pia katika Mji wa
Mpanda makao makuu ya Mkoa wa Katavi uliopo umbali wa kilometa 40 kutoka
Hifadhi ya Katavi .
Hivi
karibuni kaimu Mkuu wa Hifadhi ya Taifa ya Katavi Elias Manase
aliwaambia wandishi wa Habari wa vyombo mbalimbali wa Mkoa wa Katavi
kwamba Hifadhi hiyo inakabiliwa na changamoto mbalimbali .
Baadhi
ya changamoto hizo ni ujangili wa wanyama hasa Tembo ambao
unasababishwa na kuwepo kwa kambi za wakimbizi za Mishamo na Katumba
ambazo wanaishi Raia wa Burundi na Kongo .
Ilidai
kuwa watu wanao ishi kwenye makazi hayo wamekuwa wakiingiza silaha za
kivita na kuziingiza nchini kisha wamekuwa wakifanya ujangili wa kuuwa
Tembo na kisha wanachukua meno ya Tembo na kuyasafirisha kwenye soko la
nchi jirani.Changamoto
nyinginei ni uhaba wa miundo mbinu ndani ya Hifadhi kwani bado haiku
mizuri sana ingawa barabara zake zinapitika karibu mwaka mzima .
Manase
alitowa wito kwa watanzania kujenga utamaduni wa kutembelea Hifadhi za
Taifa kwani gharama ya kutembelea Hifadhi za Taifa ni ndogo kuliko
gharama ya mtu anayoitumia kwenye Bar kunywa pombe .
Askari
wa Hifadhi ya Katavi Joseph Mhina aliielezea Hifadhi ya Katavi kuwa
ni hifadhi ambayo ipo tofauti kabisa na Hifadhi nyingine kwani watalii
wanaotembelea Hifadhi hiyo huwa wanawaona wanyama kiurahisi kabisa kwani
watalii huwa ni wachache hivyo huwa hakuna kugombania kuwaona wanyama
kama Hifadhi nyingine .
Imeandaliwa na Blogs za Mikoa kupitia Katavi yetu Blog
0 maoni:
Chapisha Maoni