Posted by Esta Malibiche on Nov 17,2016 in NEWS
Waziri
wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akizungumza na Mkuu
wa mkoa wa Pwani Mhandisi Evarist Ndikilo mara baada ya kuwasili mkoani
pwani kwaajili ya ziara ya siku moja.
Waziri
wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akipata maelezo kwa
Kaimu Meneja Mkuu wa Kiwanda Viua Vidudu hicho,Samwel Mziray katikati ni
Mkuu wa Wilaya ya Kibaha, Assumpter Mshama.
Waziri wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akizungumza na wafanyakazi wa kiwanda cha viua vidudu, Kibaha.
Waziri
wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akipata maelezo
kutoka kwa Mkurugenzi Mtendaji wa Kiwanda cha Global Packaging, Wasonga
Otieno mkoani Pwani.
Waziri
wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akisalimia wafanyakazi
wa kiwanda cha Sayona mbele mwenye miwani ni Mkuu wa Wilaya ya
Bagamoyo, Alhaj Majjid Mwanga
Waziri
wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji Charle’s Mwijage akiwa katika picha ya
pamoja na viongozi wa Chama cha Mapinduzi wa mkoa wa Pwani. Picha na
Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Na Emmanuel Massaka, Globu ya Jamii.
Waziri
wa Viwanda Biashaa na Uwekezaji, Charle’s Mwijage amefanya ziara
kutembelea viwanda vilivyopo Mkoa wa Pwani na kuangalia maendeleo ya
mkoa huo katika sekta ya viwanda.Katika
ziara hiyo Waziri Mwijage alipotembelea kiwanda cha Viuadudu cha
kibaha, Sayona Fruits, Global Packaging kiwanda cha kuunganisha matrekta
pamoja na kiwanda cha Eveline.
Akizungumza
na waandishi wa habari baada ya kumaliza ziara hiyo, Mwijage amesema
ujenzi wa viwanda katika mkoa wa Pwani unakua kwa kasi na kuonngeza
ajira kwa watanzania.
Amesema
kitendo cha mmiliki wa kiwanda cha Sayona kuwapa wanakikjiji fursa
ya kupata elimu mpaka ngazi ya chuo kikuu na kisha kuajiliwa katika
kiwanda hicho ni uungwana ambao watafanya kazi ya kufundisha wafanyakazi
wenzao.
“Wafanyakazi
wa Sayona kupatiwa fursa ya kwenda chuo kikuu kujifunza ili kuja
kuwafundisha wenzao, kasi hiyo imenifurahisha sana” amesema Waziri
Mwijage.
0 maoni:
Chapisha Maoni