Posted by Esta Malibiche on Nov 14,2016 in NEWS
Mkurugenzi Idara ya Katiba na
Ufuatiliaji Haki Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Bw. Patience Ntwina
(aliyesimama) akitoa taarifa ya utekelezaji wa Miradi mbalimbali
inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa ujumbe wa wataalam kutoka Umoja
wa Mataifa waliotembelea Wizarani hapo leo (14/11/2016).
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Nchi
Afisi ya Rais, Katiba, Sheria, Utumishi wa Umma na Utawala Bora Zanzibar
Bw. Kubingwa Mashaka Simba akitoa taarifa ya utekelezwaji wa miradi
inayofadhiliwa na Umoja wa Mataifa kwa ujumbe wa wataalam wa Umoja huo
waliotembelea Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria Tanzania Bara leo
(14/11/2016) jijini Dar Es Salaam. Ujumbe huo umeahidi kuendelea
kufadhili miradi mbalimbali baada ya kuridhiswa na utekelezwaji wake.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mambo ya
Katiba na Sheria Prof. Sifuni Mchome akiongea katika kikao na wataalam
mbalimbali kutoka ujumbe wa Umoja wa Mataifa ambao wametembelea Wizarani
hapo leo (14/11/2016) ili kujionea namna Wizara hiyo ilivyofaidika na
kutekeleza miradi mbalimbali inayofadhiliwa na nchi wanachama wa Umoja
wa Mataifa. Wananchi hasa wasiojiweza wameweza kupata haki zao kupitia
miradi hiyo.
Sehemu ya wataalam kutoka ujumbe
wa Umoja wa Mataifa waliotembelea Wizara ya Mambo ya Katiba na Sheria
wakiwa katika kikao na Katibu Mkuu wa Wizara hiyo ( hayupo pichani) ili
kuona namna miradi inayofadhiliwa na Umoja huo inavyotekeleza.
0 maoni:
Chapisha Maoni