Posted by Esta Malibiche on Nov 16,2016 in TECHNOLOJIA
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (kushoto) akizungumza na Meneja wa
TEMESA Rukwa Mhandisi Julius Ndosi (kulia), alipotembelea kituoni hapo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme – TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu (aliyesimama) akiongea na watumishi
wa kituo cha TEMESA Rukwa alipotembelea kituo hicho hivi karibuni.
Picha zote na Theresia Mwami TEMESA Rukwa.
……………………………………………………………………
Na Theresia Mwami TEMESA Rukwa.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu amemuagiza Meneja wa TEMESA Rukwa
Mhandisi Julius Ndosi kutumia eneo la karakana ya TEMESA Rukwa kupanua
huduma zake badala ya kuwaachia watu binafsi kutoa huduma ambazo
karakana hiyo ingeweza kuzitoa.
Dkt Mgwatu ametoa agizo hilo
alipotembelea na kujionea utendaji kazi wa karakana ya TEMESA Rukwa na
kusisitiza kuwa watendaji wa kituo hicho wanatakiwa maadili na uadilifu
utekelezaji wa majukumu yao.
Ameongeza kuwa watendaji wa kituo
hicho wanatakiwa kuwa wabunifu na kutumia rasilimali zilizopo kuongeza
uwezo wa kutoa huduma zilizo bora na zinazozingatia viwango vya
kimataifa.
“Nataka wewe kama Meneja wa kituo
hiki uwe mbunifu kwa kutumia fursa zilizopo hapa Sumbawanga ili
kuzalisha mapato zaidi” alisema Dkt. Mgwatu.
Aidha Dkt. Mgwatu ametoa miezi miwili kwa Meneja huyo kukamilisha na kuwasilisha mpango wa namna ya utekelezaji wa maagizo hayo.
Mtendaji Mkuu wa Wakala wa Ufundi
na Umeme TEMESA Dkt. Mussa Mgwatu yuko katika ziara ya kikazi katika
vituo vya TEMESA Nyanda za Juu Kusini kutembelea na kukagua vituo hivyo
ili kujionea changamoto mbalimbali pamoja na utendaji kazi wake.
0 maoni:
Chapisha Maoni