Posted by Esta Malibiche on Nov 15,2016 in NEWS
Baadhi ya wagonjwa wa kisukari wa
kliniki ya Hospitali ya Mkoa wa Singida wakisubiria kufanyiwa uchunguzi
wa macho katika kuadhimisha siku ya kisukari duniani.
Daktari bingwa wa macho Mkoani
Singida Ngh’ungu Kuzenza akimfanyia uchnguzi wa macho mgonjwa wa
kisukari katika kuadhimisha siku ya kisukari duniani.
Baadhi ya wagonjwa wa kisukari wa
kliniki ya Hospitali ya Mkoa wa Singida wakisubiria kufanyiwa uchunguzi
wa macho katika kuadhimisha siku ya kisukari duniani.
……………………………………………………….
Na Grace Singida
Wagonjwa wa kisukari Mkoani
Singida leo wamefanyiwa uchunguzi wa magonjwa ya macho na daktari bingwa
wa macho katika kuadhimisha siku ya ugonjwa wa kisukari duniani ikiwa
na kauli mbiu ya ugonjwa wa kisukari na magonjwa ya macho.
Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya
rufaa ya Mkoa wa Singida Dokta Ramadhani Kabala amewaambia wagonjwa wa
kisukari waliohudhuria kufanyiwa uchunguzi wa macho kuwa maadhimisho
hayo mwaka huu yamelenga kuzuia wagonjwa wasiathirike zaidi na magonjwa
yatokanayo kisukari.
Dokta Kabala amesema ugonjwa wa
kisukari hushambulia zaidi macho, figo na moyo hivyo serikali imeweka
mkazo wa kuwafanyia uchunguzi ili kubaini tatizo ili wapatiwe matibabu
mapema au kuzuia yasitokee kabisa kwa kufuata kanuni na taratibu za
ugonjwa huo.
Ameongeza kuwa ugonjwa wa
kisukari unawakumbusha watu kuishi kwa kufuata kanuni bora za afya kama
kula mlo kamili, kula matunda badala ya juisi zilizotengenezwa
viwandani, kufanya mazoezi na kupunguza vilevi na sigara hivyo wagonjwa
wa kisukari hawana togauti na watu wengine isipokuwa wao hushauriwa
kufuata kanuni hizo kwa umakini mkubwa.
Dokta Kabala amewakumbusha
kutumia dawa kwa kufuata usahuri wa daktari wao pamoja na kuhudhuria
kliniki za kisukari kwakuwa kliniki hizo zinawasaidia katika kushauriana
namna bora ya kuishi kwa kufuata masharti wananyopewa pamoja
kuelimishanzaidi juu ya ugonjwa huo.
Naye Daktari bongwa wa macho
Mkoani Singida Dokta Ngh’ungu Kuzenza amesema utaratibu huo unasaidia
kuzuia au kupunguza madhara ya ugonjwa wa kisukari kwakuwa wengi
watatambuliwa kabla hawajafikia hatua ya kupofuka.
Dokta Kuzenza ameongeza kuwa
changamoto kubwa ni watu wengi kutopima ugonjwa wa kisukari mapema mpaka
wanapougua na hivyo kujikuta wameshaathirika macho ndipo hutafuta
huduma.
Kwa upande wake mmoja kati ya
wagonjwa wa kisukari 76 waliopata huduma ya kibingwa ya macho Bi Asha
Selemani Waziri Mkazi wa Iguguno ameema serikali imeweka utaratibu mzuri
wa kuwapima macho ili waweze kupata tiba mapema.
Bi Waziri ameiomba serikali
kuendelea kuweka utaratibu wa kuwapima wagonjwa wa kisukari magonjwa
mbalimbali kama moyo na figo huku akiwashauri wagonjwa wa kisukari
kufuata ushauri wanaopewa na wataalamu wa afya.
0 maoni:
Chapisha Maoni