Jumanne, 15 Novemba 2016

Mamlaka ya Elimu Tanzania ( TEA ) yakipiga Jeki Chuo cha Takwimu Mashariki Mwa Afrika

Posted by Esta Malibiche on Nov 15,2016 in NEWS

Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda akiongea na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)  Bw. Joel Laurent (mweyesuti) alipotembelea chuo hicho kuangalia misaada ya vifaa vya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano walivyovitoa chuoni hapo ikiwemo Ubao maalum za kufundishia (Smart Board) 4,Projecta 4 na Komputa 22, wa mwisho kulia ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe.
Makamu Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Dkt. Tumaini Katunzi na Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bw. Joel Laurent wakifuatilia maelekezo ya namna ubao maalum wa smart board unavyofanya kazi wakati wa kufundishia ikiwa ni moja ya msaada uliotolewa na mamlaka ya elimu.
Sehemu ya Komputa 22 zilizotolewa na Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) kwenye chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC).
Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA)  Bw. Joel Laurent(kulia) akimkabidhi Mkuu wa Chuo cha Takwimu Mashariki mwa Afrika (EASTC) Prof. Innocent Ngalinda moja ya projecta zitakazotumika katika kufundishia chuoni hapo, Misaada mingine ni Ubao maalum za kufundishia (Smart Board) 4 na Komputa 22,wanaoshuhudia kulia ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Mamlaka ya Elimu Tanzania (TEA) Bi. Sylvia Lupembe na kushoto ni Makamu Mkuu wa Chuo hicho Dkt. Tumaini Katunzi.

0 maoni:

Chapisha Maoni