Posted by Esta Malibiche on Nov 20,2016 in NEWS
Waziri
wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith
Kombo, akizungumza kwenye Uzinduzi wa Tamasha la Uoneshaji wa Filamu kwa
njia ya Sinema mkoani Geita, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo, Mhe.Nape Nhauye.
Uzinduzi
huo ulifanyika jana katika Ukumbi wa Desire Park Geita ambapo Taasisi
ya Sanaa Na Mazingira ya Kijani Consult Tanzania imeanzisha kampeni ya
kuonesha bure Filamu mbalimbali kwa ajili ya kufikisha elimu kwa umma
ikiwemo elimu ya Utunzaji wa Mazingira (Mabadiliko ya Tabianchi),
Ufugaji wa kuku wa kienyeji, Usalama barabarani, Madawa ya kulevya,
Madhara ya ndoa za utotoni miongoni mwa mambo mengi ya kijamii. Mradi huo umefadhiriwa na ZIFF.
Kutokana
na Mwitikio wa wanatasnia ya Filamu mkoani Geita kuonesha shauku ya
kuwa na Maonesho hayo ya Filamu, Mhe.Kombo alisema mwakani Tamasha la
Kimataifa Zanzibar pia litafanyika mkoani Geita ikiwa ni sehemu ya ZIFF
ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu kuanzishwa ZIFF.
Na BMG
Mhe.Kombo
alisema mwakani Tamasha la Kimataifa Zanzibar pia litafanyika mkoani
Geita ikiwa ni sehemu ya ZIFF ni sehemu ya kusherehekea miaka 20 tangu
kuanzishwa ZIFF.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fessoo, akizungumza kwa
niaba ya Serikali kwenye uzinduzi huo ambapo aliwahakikishia Wanatasnia
ya Filamu mkoani Geita na nchini kwa ujumla kwamba Serikali itahakikisha
inaboresha zaidi sanaa ya filamu ikiwemo kuendelea kutoa mafunzo ya
filamu kwa wanatasnia hiyo ili filamu zinazozalishwa ziwe na ubora.
Aidha
alidokeza kwamba Serikali inatoa baraka zote kuhusiana na Tamasha la
Kimataifa la Filamu Zanzibar, pia kufanyika mkoani Geita hapo mwakani.
Mkuu
wa Mkoa wa Geita, Meja Jenerali Mstaafu, Ezekiel Kyunga, akizungumza
kwenye Uzinduzi wa Uoneshaji wa Filamu mkoani Geita, ambapo alisisitiza
kwamba sanaa ni ajira hivyo wanatasnia hiyo watumie fursa mbalimbali
ikiwemo mafunzo yanayotolewa na serikali ili kuboresha zaidi kazi zao.
Katibu
wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Robert Manondolo,
akizungumza kwenye uzinduzi huo ambapo alibainisha kwamba ZIFF imekuwa
ikitoa ufadhiri kwa taasisi mbalimbali nchini ikiwemo Taasisi ya Kijani
Consult kwa lengo la kuziwezesha kufikisha elimu kwa umma kwa njia ya
kuonesha filamu bure na kufikisha elimu iliyokusudiwa.
Katibu
Tawala Wilayani Geita, Thomas Dimme, akizungumza kwenye uzinduzi wa
Tamasha la Uoneshaji wa Filamu bure mkoani Geita ili kufikisha elimu
mbalimbali ikiwemo Ufugaji na utunzaji wa Mazingira.
Herman Matemu (aliyesimama) ambaye ni Kaimu Afisa Tawala mkoa wa Geita, akisalimia kwenye uzinduzi huo.
Kulia
ni Kuka Kahindi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa na
Mazingira ya Kijani Consult ya mkoani Geita, akisoma risala kuhusiana na
Mradi wa Uoneshaji Filamu Bure mkoani Geita.
Alisema
mradi huo umelenga kutoa chachu kwa wanajamii kutumia fursa mbalimbali
ikiwemo ufugaji kujipatia kipato badala ya kutegemea shughuli moja kama
vile madini. Pia kuwahimiza kujiepusha na uharibifu wa mazingira. Yote
hayo pamoja na mengine yanafikishwa kwa wananchi kwa njia ya filamu.
Mgeni
Rasmi, Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF,
Mhe.Mahmood Thabith Kombo (kulia) akipokea taarifa ya mradi wa uoneshaji
wa filamu bure mkoani Geita kutoka kwa Kuka Kahindi ambaye ni Kaimu Mkurugenzi wa Taasisi ya Sanaa na Mazingira ya Kijani Consult ya mkoani Geita (kushoto).
Mkuu
wa idara ya Habari, Kijani Consult Tanzania, Rose Mweko, akitoa salamu
zake kwenye uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure katika maeneo ya
wazi mkoani Geita.
Kutoka
Kushoto ni Mwakilishi wa Balozi wa Denimark nchini Tanzania, Dotto
Kahindi, Katibu Mtendaji Bodi ya Filamu Tanzania, Bi.Joyce Fessoo na Mgeni
Rasmi, Waziri wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia
ni Mwenyekiti wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF,
Mhe.Mahmood Thabith Kombo, wakifuatilia kwa makini zoezi la uzinduzi wa
mradi wa Kuonesha Filamu bure mkoani Geita ili kufikisha elimu kuhusu
masuala mbalimbali kwa wanajamii.
Meza kuu wakifuatilia matukio mbalimbali kwenye uzinduzi wa mradi wa Kuonesha Filamu bure mkoani Geita
Wageni mbalimbali waliohudhuria uzinduzi huo
Maafisa Habari mkoani Geita wakifuatilia uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure mkoani Geita
Wageni mbalimbali wakifuatilia uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure mkoani Geita
Wanahabari mkoani Geita wakifuatilia uzinduzi wa mradi wa kuonesha filamu bure mkoani Geita
Wanatasnia wa Filamu mkoani Geita
Burudani za asili mkoani Geita
Burudani za asili zikiendelea
Baadhi
ya wakazi wa mkoa wa Geita wakifuatilia Uzinduzi wa Mradi wa Uoneshaji
wa Filamu bure mkoani humo ili kufikisha elimu ya masuala mabalimbali
ikiwemo uharibifu wa mazingira pamoja na ufugaji kwa njia ya filamu
Mgeni Rasmi, Waziri
wa Afya katika Serikali ya Mapinduzi Zanzibar, ambaye pia ni Mwenyekiti
wa Tamasha la Kimataifa la Filamu Zanzibar ZIFF, Mhe.Mahmood Thabith
Kombo (mwenye kofia) pamoja na
viongozi wengine, wakiwa kwenye picha ya pamoja na watoto walioshiriki
shindano fupi la kucheza muziki kwenye Uzinduzi wa Mradi wa kuonesha
Filamu bure mkoani Geita.
Mgeni
Rasmi Mhe.Kombo (mwenye kofia) pamoja na viongozi wengine, wakiwa
kwenye picha ya pamoja na watoto, Maisala Ibrahimu anayesoma kidato cha
pili shule ya Sekondari Kangalala (ke) na Joshua Tito anayesoma darasa
la kwanza shule ya msingi Kivukoni Geita (Me) ambao walioonesha vipaji
vya hali ya juu katika kucheza muziki.
ZIFF
imetoa fursa ya kuwanunulia mavazi ya shule watoto hao huku pia
wakipata fursa ya Kuhudhuria Tamasha la Kimataifa la Filamu katika
Visiwa vya Zanzibar hapo mwakani.
Bonyeza HAPA Kutazama picha za kikao cha Wanatasnia ya Filamu mkoani Geita na Bodi ya Filamu Tanzania.
0 maoni:
Chapisha Maoni