Posted by Esta Malibiche on Nov 29,2016 in NEWS
Na Adili Mhina, Kigoma
Wizara
ya Fedha na Mipango -Tume ya Mipango kwa kushirikiana na Serikali ya
Ubelgiji inaendesha mafunzo ya maandalizi ya miradi ya maendeleo kwa
ajili ya ufadhili wa washirika wa maendeleo kwa Mkoa wa kigoma.
Akifungua
mafunzo hayo yanayoendelea mjini kigoma na kuwashirikisha Makatibu
Tawala, Wakurugenzi na wataalam wa sera na mipango kutoka Halmashauri
zote za Mkoa wa kigoma, Kaimu Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi
Florence Mwanri alieleza kuwa Serikali ya Ubelgiji ambayo ndio
iliyofadhili mafunzo hayo kuwa imefanya jitihada kubwa katika kufadhili
miradi mbalimbali katika Mkoa wa Kigoma.
“Tunaishukuru
sana Serikali ya Ubelgiji kwani kwa kipindi kirefu imekuwa ikifanya
kazi kubwa katika kufadhili miradi ya maendeleo hususan kwenye sekta za
kilimo na maji ambapo kwa kiwango kikubwa imesaidia kuboresha maisha ya
wananchi wa mkoa huu,” alieleza Bibi Mwanri.
Alisisitiza
kuwa licha ya mafanikio yaliyopatikana kupitia miradi iliyotekelezwa na
inayoendelea kutekelezwa na Serikali ya Ubelgiji katika Mkoa wa Kigoma
zipo changamoto kadhaa ambazo zimeonekana kupunguza ufanisi wa miradi
husika.
Miongoni
mwa changamoto hizo ni; rushwa, kiwango kisichoridhisha cha uratibu wa
utekelezaji wa miradi, uwakilishi duni katika kamati za utekelezaji wa
miradi na ugumu wa kupata taarifa za utekelezaji wa miradi mbalimbali ya
maendeleo.
Changamoto
nyingine ni pamoja na miundombinu mibovu hususan barabara na umeme
ambayo inachangia kutokuvutia wataalam kuishi katika mkoa wa Kigoma, na
uhaba wa utaalam katika maandalizi, kutekeleza na kusimamia kwa ufanisi
fedha zinazotumika kugharamia miradi ya maendeleo.
Mwanri
aliongeza kuwa baada ya kubaini changamoto hizo, Tume ya Mipango kwa
kushirikiana na Serikali ya Ubelgiji iliona umuhimu wa kutoa mafunzo ili
kuongeza uelewa wa wataalam katika kuainisha, kuchagua, kuchambua,
kutafuta njia sahihi za ugharamiaji, kusimamia utekelezaji, na kufanya
ufuatiliaji na tathmini ya miradi ya maendeleo.
Nae
Mratibu wa mafunzo hayo Bw. Paul Sangawe alifafanua kuwa katika
kutekeleza Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2016/17-2020/21)
uwekezaji wa Umma umeongezeka ambapo kwa sasa Serikali inatumia
Shilingi za kitanzania trilioni 11.8 kila mwaka, na katika kipindi cha
miaka mitano ijayo shilingi Trilioni 59 zinatazamiwa kutumika kugharamia
miradi ya maendeleo.
“Ni
muhimu kuelewa kuwa ugunduzi wa gesi, madini, nk kunaendana na ongezeko
la mapato kwa Serikali huku matumizi katika eneo la miradi ya maendeleo
nayo yakiongezeka. Hivyo, ni vyema kijiandaa mapema ili kuhakikisha
kuwa fedha zitakazopatikana zinatumika kwa ufanisi na kuleta matokeo
tarajiwa,” alieleza Sangawe.
Kwa
mujibu wa Sangawe, matarajio katika mafunzo hayo ni pamoja na; kupata
maoni kutoka kwa washiriki kwa ajili ya maandalizi ya programu ya
ushirikiano wa maendeleo baina ya Serikali ya Tanzania na Ubelgiji
(2017- 2021), kuongezeka kwa ufanisi wa utekelezaji, ufuatiliaji na
tathmini ya miradi ya maendeleo na kuhakikisha kuwa maandiko yote ya
miradi ya maendeleo yanazingatia Mwongozo wa Usimamizi na Uwekezaji wa
Umma.
Sangawe
ambaye pia anasimamia Klasta ya Biashara za Kimataifa na Mahusiano ya
Uchumi Tume ya Mipango amewahakikishia washiriki wa mafunzo hayo kuwa
washirika wa maendeleo wanaunga mkono jitihada za Serikali katika
kuimarisha uchumi na hasa katika utekelezaji wa miradi ya maendeleo ili
kuhakikisha kuwa Tanzania inafikia malengo ya Dira ya Maendeleo ya Taifa
ya kuwa nchi ya kipato cha kati ifikapo 2025.
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango, Florence Mwanri akitoa hotuba ya
Ufunguzi wa mafunzo ya miradi ya maendeleo kwa ajili ya ufadhili wa
washirika wa maendeleo kwa Mkoa wa kigoma. Kulia ni mwakilishi wa Katibu
Tawala Mkoa wa kigoma Bw. Samwel Tenga, wa kwanza kushoto ni Kaimu
Naibu Katibu Mtendaji Klasta ya Uchumi Jumla kutoka Tume ya Mipango,
Dkt. Lorah Madete na pembeni yake (mwenye tai) ni Mratibu wa mafunzo
hayo Bw. Paul Sangawe.
Baadhi
ya washiriki wa mafunzo ambao ni Makatibu Tawala, Wakurugenzi na
wataalam wa sera na mipango kutoka Halmashauri zote za Mkoa wa Kigoma
wakiendelea wakifuatilia mafunzo.
Mratibu
wa Mafunzo Bw. Paul Sangawe akitoa maelezo juu ya utayari wa washirika
wa maendeleo katika kufadhili miradi ya maendeleo nchini. Kulia ni Kaimu
Katibu Mtendaji Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri na Kushoto ni Dkt.
Lorah Madete kutoka Tume ya Mipango.
Mkufunzi
wa Mafunzo kutoka Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Dkt. John Mduma akitoa
mafunzo juu ya maandalizi ya miradi ya maendeleo kwa ajili ya ufadhili
wa washirika wa maendeleo.
Baadhi ya wadau wa mafunzo wakimsikiliza mkufunzi (hayupo picha ni) wakati wa mafunzo mjini Kigoma.
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri (Wapili kutoka
kulia kwa waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na Wakufunzi kutoka
Chuo Kikuu cha Dar es Salaam pamoja na Matibu Tawala wa Wilaya za
Kigoma, Kasulu, Kibondo, Uvinza na Kakonko. Wa kwanza kulia (waliokaa)
ni mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa wa Kigoma, Bw. Samwel Tenga, wengine
ni viongozi kutoka Tume ya Mipango.
Kaimu
Katibu Mtendaji wa Tume ya Mipango Bibi Florence Mwanri (Wapili kutoka
kulia kwa waliokaa) akiwa na wakurugenzi wa Mipango kutoka Halmashauri
za Mkoa wa Kigoma.
Picha
ya pamoja kati ya Kaimu katibu Mtendaji, Tume ya Mipango, Bibi Florence
Mwanri wa pili kutoka kulia (waliokaa) akiwa katika picha ya pamoja na
maafisa Mipango, Wachumi, na Watakwimu kutoka Halmashauri za mkoa wa
Kigoma. Wa kwanza kulia (waliokaa) ni mwakilishi wa Katibu Tawala Mkoa
wa Kigoma, Bw. Samwel Tenga wengine ni viongozi kutoka Tume ya Mipango.
0 maoni:
Chapisha Maoni