Jumanne, 15 Novemba 2016

MKUU WA MKOA WA MBEYA AMOS MAKALLA ATANGAZA NEEMA KWA WAFANYABIASHARA NA WAJASIRIAMALI.

Posted by Esta Malibiche on Nov 15,2016 in NEWS
MKUU wa mkoa wa Mbeya Amos Makalla leo ameshuhudia utiaji saini ya utoaji Mafunzo kwa wafanyabiashara kuhusu Ufungishaji bidhaa na barcode kati ya kampuni GS1 Tanzania na Halmashauri zote za mkoa wa mbeya.

Kauli hiyo ameitoa mapema leo hii wakati wa utiaji saini makubaliano  na wakurugenzi kuwezesha mafunzo ya Barcode huku akiwasihi  wafanyabiashara na wajasiliamali  kujitokeza kwa wingi mara mafunzo yatakapoanza.

‘’’’Ninawaomba wafanyabiashara na wajasiliamali wa Mkoa wa Mbeya mjitokeze kwa wingi mara mafunzo haya yatakapoanza ili muweze kupata Elimu ya kutosha kuhusu namna ya kuyafikia masoko yalipo ndani na nje ya nchi yetu’’’’’Alisema Makalla

Kwa upande wake Mkurugenzi wa GS1 Tanzania Fatuma Kange amepongeza jitihada za Mkuu wa Mkoa wa Mbeya,kwa jitihada zake za kuhakikisha wafanyabiashara na wajasiliamali wanapata mafunzo yanayotarajia kuanza mwezi Januari 2017.

Kange alisema Mkoa wa Mbeya utakuwa Mkoa wa mfano na ana imani kuwa mikoa mingine itaiga jitihada za kuwasaidia wananchi kujikwamua kiuchumi na zaidi kuifanya Tanzania yenye viwanda kwa vitendo.

Alisema  Mkoa wa Mbeya,akiwa na lengo la kuwasaidia wajasiariamali na wafanyabiashara kuboresha bidhaa zao na kuyafikia utiaji saini ni utekelezaji wa maagizo ya Mkuu wa mkoa ili kuweza kuyafikia masoko  ya ndani na nje ya nchi.
 
‘’’’’’Mafunzo haya yatawaongezea wajasiriamali Elimu ya ufungaishaji wa bidhaa na itawezesha kuyafikia masoko ndani na nje ya nchi’’’’’’Alisema Kange



 




0 maoni:

Chapisha Maoni