Posted by Esta Malibiche on Nov 20,2016 in NEWS
Mkurugenzi
Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard
Maboko akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam juzi,
ambapo aliwaasa wananchi kuchukua uamuzi wa kupima afya zao na kupatiwa
matibatu. Kulia ni Mwenyekiti wa Tume hiyo, Dk. Hedwiga Swai.
……………………………………………..
Na Dotto Mwaibale
WANANCHI wametakiwa kupima kila wakati na kuendelea kutumia kinga ili kujiepusha na maambuki mapya ya VVU.
Mwito
huo umetolewa na Mkurugenzi Mtendaji wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi
Tanzania (TACAIDS), Dk. Leonard Maboko katika kikao cha makamishina
wapya wa tume hiyo kilichoketi jijini Dar es Salaam juzi.
“Tunapaswa kuwa ni mikakati endelevu ya kupambana na ugonjwa wa ukimwi kwani bado kunachangamoto kubwa” alisema Maboko.
Maboko alisema watanzania wasidanganyike kuwa ukimwi umekwisha ugonjwa huo bado upo na ni changamoto kubwa.
Alisema
changamoto kubwa ya ugonjwa huo bado ipo katika baadhi ya mikoa hasa
ile ya nyanda za juu kama Iringa na Njombe hivyo wananchi wasibweteke
kuwa ugonjwa huo umekwisha.
Alisema kwa Tanzania Bara kunamaambukizi ya asilimia 5.3 sawa na watu milioni mbili waliopata maambukizi.
0 maoni:
Chapisha Maoni