Posted by Esta Malibiche on NOV 12,2016 in NEWS
Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza, Mary Tesha (kushoto), akipokea
cheti cha utambuzi kutoka kwa Katibu Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini,
Joyce Fesso (kulia), wakati wa ufungaji wa Mafunzo kwa Wasanii wa Filamu
mkoani Mwanza yaliyoanza juzi Novemba 10 na kutamatika leo Novemba
12,2016 katika ukumbi wa ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Mhe.Tesha amemwakilisha mkuu wa mkoa wa Mwanza, John Mongella.
Na BMG
Na George Binagi-GB Pazzo
Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza,Mary Tesha, amemtaka Afisa
Utamaduni mkoani mkoani hapa, kuhakikisha maadhimio yaliyoafikiwa na
wasanii wa filamu mkoa wa Mwanza yanaanza hatua za utekelezaji ndani ya
siku saba.
Nje ya
hotuba ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Tesha amesema Afisa Utamaduni mkoa wa
Mwanza, James Willium, kwa kushirikiana na maafisa utamaduni wa
halmashauri zote za mkoa wa Mwanza wanapaswa kuhakikisha wanatoa
mikakati ya utekelezaji wa maadhimio yaliyotolewa kwenye mafunzo hayo
ili utekelezaji huo uanze mara moja.
Miongoni
mwa maadhimio saba ya wasanii walioshiriki mafunzo hayo ambayo
yamewasilishwa na Mwakilishi kutoka Chama cha Waongozaji wa Filamu
mkoani Mwanza, Mwanaharusi Hela, ni pamoja na uongozi (Serikali) wa mkoa
wa Mwanza kusaidia upatikanaji wa kituo cha sanaa (studio ya kisasa)
kwa ajili ya kurekodia filamu na vipindi vya runinga pamoja na
kushirikishwa kwenye dhifa mbalimbali za kimkoa na kitaifa ili kuonesha
kazi sanaa zao.
Katika
mafunzo hayo, Mkurugenzi wa Taasisi ya Utafiti wa Sanaa Asilia, Mzee
Fumbuki Lubasa, ametoa bure kiwanja chenye ukubwa wa hekta 50 kwa 40
kilichopo Nyegezi Jijini Mwanza ili wasanii wa filamu mkoani Mwanza
wajengewe studio kwa ajili ya kurekodia kazi zao ambapo Mfuko wa
Pensheni wa PPF umeonesha nia ya dhati ya kufadhiri ujenzi wake.
Zaidi
ya washiriki 300 wamepata mafunzo hayo ambapo Katibu Mtendaji wa Bodi ya
Filamu nchini, Joyce Fesso, amesema yamelenga kuwajengea weledi wadau
wa filamu wakiwemo waigizaji, waongozaji na wahariri, kutengeneza kazi
zenye ubora, kutambua majukumu ya bodi hiyo, hakimili na hakishirikishi
ili kukuza soko la filamu na hivyo kunufaika na kazi zao.
Meneja
Mawasiliano kutoka Mamlaka ya Mawasiliano nchini TCRA, Innocent Mungy
(kushoto), akipokea cheti cha utambuzi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya
Nyamagana, Mary Tesha, aliyemwakilishwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye
ufungaji wa mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo.
Rais
wa Shirikisho la Filamu nchini, Simon Mwakifwamba (kushoto), akipokea
cheti cha utambuzi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha,
aliyemwakilishwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa mafunzo kwa
wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo.
Mwenyekiti
wa Chama cha Waigizaji mkoani Mwanza, Ramadhan Mustapha (kushoto),
akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary
Tesha, aliyemwakilishwa mkuu wa Mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa
mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo.
Mwakilishi
kutoka Chama cha Waongozaji wa Filamu mkoani Mwanza, Mwanaharusi Hela
(kushoto), akipokea cheti cha ushiriki wa mafunzo kutoka kwa Mkuu wa
Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha.
Mshauri
wa sanaa ya Filamu mkoani Mwanza ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya
Utafiti wa Sanaa Asilia, Mzee Fumbuki Lubasa (kushoto), akipokea cheti
cha utambuzi kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Nyamagana, Mary Tesha.
Mzee
Lubasa ametoa bure kiwanja chenye ukubwa wa hekta 50 kwa 40 kilichopo
Nyegezi Jijini Mwanza kwa ajili ya wasanii wa filamu mkoani Mwanza
kujengewa studio ya kisasa kwa ajili ya kurekodia kazi zao.
Kushoto
ni mmoja wa washiriki wa mafunzo ya sfilamu yaliyoandaliwa na bodi ya
filamu nchini, akipokea cheti cha ushiriki kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya
Nyamagana, Mary Tesha.
Mkuu
wa Wilaya ya Nyamagana mkoani Mwanza,Mary Tesha, akifunga Mafunzo kwa
wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo, kwa niaba ya mkuu wa mkoa wa
Mwanza.
Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fessoo, akizungumza wakati wa
ufungaji wa mafunzo ya filamu mkoani Mwanza hii leo. Amesema lengo la
mafunzo hayo ni kuwajengea weledi wasanii wa filamu ili kutengeneza kazi
bora.
Mshauri
wa Utamaduni mkoani Mwanza, James Willium, akizungumza wakati wa zoezi
la ufungaji wa mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo
Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo akitoa mchango wake kuhusu uendelezaji wa soko la filamu mkoani Mwanza.
Mwakilishi
kutoka Chama cha Waongozaji wa Filamu mkoani Mwanza, Mwanaharusi Hela ,
akifuatilia mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza.
Msanii
wa nyimbo za asili, Chifu Mwananzengo (wa pili kulia) pamoja na
wachezaji wake, akitoa burudani kuhusu mkoa wa Mwanza kwenye ufungaji wa
mafunzo kwa wasanii wa filamu mkoani Mwanza hii leo
Washiriki
wa mafunzo ya filamu mkoani Mwanza wakifuatilia burudani kutoka kwa
msanii wa nyimbo za asili, Chifu Mwananzengo kutoka wilayani Kwimba hii
leo
Washiriki wa mafunzo ya filamu mkoani Mwanza, wakifuatilia mada kwenye mafunzo hayo hii leo kabla ya mafunzo hayo kufungwa.
Washiriki
wa mafunzo ya filamu mkoani Mwanza, wakifuatilia mada kutoka kwa Katibu
Mtendaji wa Bodi ya Filamu nchini, Joyce Fesso.
Picha ya pamoja
0 maoni:
Chapisha Maoni