Posted by Esta Malibiche on Nov 28,2016 in MICHEZO
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye (katikati) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kabla ya makabidhiano ya picha ya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli
iliyochorwa na kikundi cha Angavu Youth Group leo jijini Dar es Salaam.
Picha hiyo imekabidhiwa kwa Waziri huyo kwa niaba ya Mhe. Rais. kushoto
ni Mwenyekiti wa Angavu Youth Group Bw. Athumani Salum na kulia ni
Katibu wake Bi. Oliver Charles.Picha na Anitha Jonas – MAELEZO
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akisikiliza kwa makini
hotuba iliyokuwa ikisomwa na Katibu wa Angavu Youth Group Bi.Oliver
Charles (katikati) wakati wa makabidhiano ya picha ya Mhe. Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo jijini Dar
es Salaam.
Waziri wa Habari, Utamaduni,
Sanaa na Michezo Mhe.Nape Moses Nnauye (kulia) akipokea picha ya Mhe.
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli kutoka
kwa Mwenyekiti wa Angavu Youth Group Athumani Salum (kulia) leo jijjini
Dar es Salaam. Picha hiyo imechorwa kwa ustadi na kikundi cha Angavu
Youth Group.
Muonekano wa picha ya Mhe. Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli iliyoichora
kwa ustadi na kikundi cha Angavu Youth Group ambapo imekabidhiwa leo
jijini Dar es Salaam kwa Waziri wa Habari,Utamaduni,Sanaa na Michezo
Mhe.Nape Moses Nnauye kwa niaba ya Mheshimiwa Rais.
0 maoni:
Chapisha Maoni