Alhamisi, 24 Novemba 2016

MKUU WA MKOA WA MBEYA AMOS MAKALLA ATANGAZA MKAKATI WA KULIWEKA SAFI JIJI LA MBEYA,KUPUNGUZA FOLENI NA AJALI

Posted by Esta Malibiche on Nov 24,2016 in NEWS

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla akizungumza na wananchi wa mkoa wa Mbeya leo hii wakati wa kufungua maadhimisho ya wiki ya  Usalama Barabarani

Mkuu wa Mkoa wa Mbeya Amos Makalla leo amefunga maadhimisho ya wiki ya  usalama barabarani mkoa wa Mbeya na kutangaza mkakati kabambe ikiwemo kuondoa foleni,kupunguza ajali  za barabaranina kuliweka jiji katika hali ya usafi.
 

Akizungumza wakati na wananchi wa mkoa wa Mbeya katika ufunguzi huo,alisema kuwa  uendeshaji wa vyombo vya Moto bila kuwa na leseni kuwa ndiyo chanzo cha kuongezeka kwa ajali nchini.

Amewaomba wananchi kuheshimu sheria za barabarani na amepiga marufuku shughuli Ndani ya road Reserve

Makalla alisema Bodaboda, Bajaji , Taxi na Daladala waheshimu Route na vituo walivyopangiwa,huku akiwataka waendesha vyombo vya Moto kuwa na leseni.



‘’’’Operesheni weka jiji la Mbeya imeanza wiki hii na kupitia maadhimisho YA wiki YA usalama barabarani amewataka madereva wa bajaji, daladala, bodaboda na taxi kuheshimu route na vituo walivyopangiwa hii itasaidia kuweka jiji safi lakini utaondoa Foleni na bughudha kwa watumiaji wengine wa Barabara’’’alisema Makalla



 







0 maoni:

Chapisha Maoni