Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla, ameendelea na usimamizi wa Operesheni Maalum ya kufuatilia na kuufumua mtandao wa Viroba na Pombe feki na haramu nchini ambapo leo Novemba 16.2016 ameweza kukifungia kiwanda cha Afro American kinachozalisha pombe aina ya ZED.
Katika tukio hilo, Dk. Kigwangalla ambaye pia aliongozana na timu ya wataalam mbalimbali na maafisa usalama  amelazimika kukifunga kiwanda  hicho cha Afro American kinachozalisha viroba aina ya Zed, Dollars na vinginevyo ambavyo vimekutwa havina vibali vya TFDA na havina usajili wa TFDA, havina Batch Number ya kutambua uhalali wa uzalishaji wak.
Pia pombe hizo pia zilibainika kutokuwa na  tarehe ya kuzalishwa na wala ya ku-expire hali ambayo ni vigumu kutambua ubora wake na idadi yake halisi kwa maksudi ya kulipa kodi ya serikali.
Hata hivyo, wenye kiwanda walibainika kutokuwa utunzaji wa kumbukumbu wala  rekodi za uzalishaji huku wakikili kuwa mitambo yao haina uwezo wa kuweka batch number.
Tukio hilo ni la mwendelezo maalum kufuatia zoezi la jana Novemba 15.2016 Dk. Kigwangalla kuendesha operesheni hiyo maalum na kubaini uwepo wa bidhaa hizo sokoni na hivyo kuagiza wataalamu wafuatilie ili kubaini viwanda zaidi vinavyotengeza pombehizo ikiwemo zile feki na wale wanaokiuka taratibu kwani bidhaa hizo baadhi yake zimekuwa zikisababisha matatizo makubwa kwa afya za binadamu.
viroba
KigwangalaNaibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dkt. Hamisi Kigwangalla.