Posted by Esta Malibiche on Nov 12,2016 in NEWS
Na
Esta Malibiche
Iringa
MKUU
wa mkoa wa Iringa Amina Masenza amezindua Oparesheni Komaza,ambayo
takribani Wanamgambo zaidi ya200 wameshiriki katika zoezi la oparesheni komaza
mkoani Iringa .
Mafunzo
hayo yataenda sanjali na zoezi la kulenga shabaha ambalo litachukua siku nne
porini likihusisha mazoezi ya ukakamavu pamoja na mazoezi mengine ya kijeshi
kwa wanamgambo hao.
Akizungumza
wakati wa kuzindua zoezi hilo lililofanyika katika viwanja vya shule ya msingi
Mlandege Manispaa ya Iringa Mkoani hapa likiwa limekusanya vijana toka vijiji
vya Mboliboli, Wasa, Idodi na kwingineko wilayani Iringa Mkuu wa Mkoa wa Iringa
Amina Masenza amewataka viongozi wote wa siasa waache mara moja kuingilia
shughuli yeyote inayohusishwa na jeshi la Mgambo,na kusema kuwa jeshi la mgambo
kwani jeshi halina itikadi yoyote ya kichama
.
Masenza
alisema kuwa lengo la mafunzo hayo ni kuwajengea vijana uwezo wa kuwa Imara
kiafya, waweze kupambana pamoja na kuwaandaa kuwa vijana wazalendo katika jamii
na kwa taifa kwa ujumla.
‘’’’Jeshi
la mgambo lina msaada mkubwa sana katika ulinzi wa taifa hivyo ni muhimu sote
tukachukulia mafunzo haya kama chachu ya maendeleo, ulinzi na usalama hivyo ‘’’Alisema Masenza
Katika
kuhakikisha zoezi linaenda sawa Mkuu wa Mkoa Amina Masenza alitoa gunia la
mahindi ili likasaidie chakula kwa wanamgambo wakiwa mafunzoni na akatoa
shukrani kwa wadau na kusema kuwa sasa kuna uhakikia kuwa vijana hawatapata
shida kwenye suala la chakula.
Awali
akimkaribisha Mkuu wa mkoa wa Iringa,Mkuu wa wilaya ya Iringa Richard Kasesela
aliyataka makampuni ya ulinzi kuanza kutoa ajira kwa vijana waliopitia mgambo
ili kupunguza idadi ya vijana wasio na ajira mtaani.
“Tumeamua kuwa na kikosi mahili ili kisaidie
kupambana na majangili pamoja na wahamiaji haramu ambao wamekuwa tishio katika
wilaya yetu”
Kwa
upande wake mshauri wa mgambo wilaya ya Iringa Afande J.M Kita amewashukuru
baadhi wa wadau kwa misaada waliyotoa katika kuhakikisha zoezi hilo
linafanikiwa.
Kita
aliwataja baadhi ya wadau waliochangia kuwa ni pamoja na ndugu Sallim Asas
aliyetoa shilingi milioni moja ambayo imeziingizwa moja kwa moja katika
kughalamia chakula kwaajili ya vijana hao, naye meneja wa TANROAD wilaya ya
Iringa ametoa Mchele kwaajili ya vijana
hao. Kisha Afande KITA akatoa rai kwa wadau ambao wataguswa kusaidia maana bado
kuna uhitaji wa msaada wa hali na maali ili kufanikisha ziezi hilo.
0 maoni:
Chapisha Maoni