Katibu
Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu anayeshughulikia masuala ya Sera na Uratibu
Dkt.Hamisi Mwinyimvua amekutana na Kamati ya Taifa ya Uratibu wa Maafa
kwa lengo la kujadili masuala mbalimbali ya Menejimenti ya Maafa.
Mkutano
huo ulifanyika Novemba 04, 2016 katika Ofisi ya Waziri Mkuu Dar es
Salaam na kuhusisha wadau mbalimbali kutoka Wizara, Idara na Taasisi za
umma zinazohusika na shughuli za maafa.
Dkt.
Mwinyimvua alieleza kuwa katika kutimiza malengo ya Kamati hiyo, Ofisi
ya Waziri Mkuu inajukumu la kuandaa mkutano wa Kamati ya Taifa wa
Uratibu wa Maafa Nchini ili kukidhi matakwa ya kisheria.
“Ofisi
ya Waziri Mkuu inawajibu wa kuratibu mkutano huo ili kuhakikisha
unafanyika kwa mujibu wa sheria ya maafa namba 9 ya mwaka 1990 na
inaelekeza kikao kiwe kinafanyika kila robo ya mwaka au pale inapotokea
dharura/maafa yatakayolazimu kikao kufanyika,” alisema Dkt.Mwinyimvua
Miongoni
mwa mambo yaliyojadiliwa katika mkutano huo ni pamoja na kupata taarifa
za kukabiliana na maafa mbalimbali nchini, kuanzishwa kwa Wakala wa
Usimamizi wa Maafa na kuanzishwa kwa Kituo cha Operesheni na Mawasilano
ya Dharura (Emergency Operation and Communication Center).
Vile
vile Wajumbe wa mkutano huo walipata fursa ya kujadili masuala ya
Menejimenti ya Maafa hususani katika masuala ya Mpango wa Taifa wa
Ufuatiliaji na Uokoaji, taarifa za Hali ya Hewa nchini na kutoa
maelekezo ya hatua za kuchukuliwa na wadau mbalimbali na wananchi kwa
ujumla na kujadili Utekelezaji wa Mfumo wa kidunia wa Uboreshaji na
Uimarishaji wa Utoaji na Matumizi ya Huduma za Hali ya Hewa.
0 maoni:
Chapisha Maoni