Ijumaa, 4 Novemba 2016

MILIONI 579.9 KUTENGENEZA BARABARA HALMASHAURI YA MUFINDI IRINGA

Posted by Esta Malibiche on Nov 4,q2016 in NEWS






 Na Esta Malibiche
 Mufindi


HALMASHAURI  ya Wilaya ya Mufindi imesaini mikataba 06 yenye thamani ya shilling milioni 579.8 na wakandarasi 06 tofauti kwa lengo la kufanya  matengenezo  ya barabara mbalimbali zilizopo ndani ya Halmshauri hiyo,zenye urefu waKm 70 zilizopo kwenye kata na vijiji  vilivyo katika Halmashauri hiyo.

Akizungumza jana wakati wa hafla fupi ya utiaji saini wa mikataba hiyo kati ya Halmashauri na wakandarasi waliopewa kazi ya matengenezo hayo, Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi Mh. Festo Mgina amewataka wakandarasi  kutekeleza miradi hiyo kwa kuzingatia vigezo vinavyokubalika kwenye kandarasi walizozisaini ikiwa nipamoja na kutengeneza kwa wakati na kuzingatia ubora utakaoendana na thamani ya Fedha watakazo lipwa.

Mgina alisema barabara zinazotarajiwa kufanyiwa matengenezo wakati wowote kuanzia hivi  sasa kuwa  ni pamoja na barabara ya Mdabulo- Lulanda kwa urefu wa km 9.0, barabara ya Mninga – Mkalala – Kasanga km 9.0, barabara ya Tambalang’ombe – katwanga km 10, barabara ya Vikula – kilosa Mufindi km 12, barabara ya Lutheran – Isupilo km 7.5 huku ile ya mtili- ifwagi mpaka Mkuta ikifanyiwa matengenezo kwa km 13.

Kwa upande wake Mkurugenzi mtendaji wa Halmshauri ya Wilaya ya Mufindi Dkt. Riziki Shemdoe alisema kuwa,kuanzia sasa ofisi yake   itakuwa ikisaini mikataba yote kwa uwazi,huku akiwatoa hofu wakandarasi na kusema kuwa malipo ya  Fedha zao yatalipwa kwa wakati mara tu watakapokamilisha kazi zao.

‘’’’’’Ninawaomba tufanye kazi kwa kiwango kinachotakiwa na tulichokubaliana,Sitakuwa tayari kumlipa mkandarasi atakaediriki kutengeneza barabara chini ya kiwango na kinyume cha makubaliano yetu’’’’’Alisema Shemdoe

0 maoni:

Chapisha Maoni