Posted by Esta Malibiche on Nov 5,2016 in NEWS
Msemaji Mkuu wa Kambi Bungeni katika Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Joseph Mbilinyi akiwasilisha hotuba ya kambi hiyo kuhusu Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016 |
Na Mwandishi wetu,
Dodoma
Kambi Rasmi ya
upinzani Bungeni yaikubali Bodi ya Ithibati, Baraza Huru la Habari pamoja na
Bima ya Afya kwa waandishi wa habari nchini.
Akiwasilisha maoni ya
Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni mjini Dodoma, Msemaji Mkuu wa Kambi hiyo katika
Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Joseph Mbilinyi amesema kuwa Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari wa 2016
unamaufaa kwa wanahabari nchini.
“Kifungu cha 58
kinatoa jukumu na kuwataka waajiri wa waandishi wa habarikuhakikisha kuwa
waandishi wa habari wanakuwa na bima ya afya pamoja na kuhakikisha kuwa
wanachangia katika mifuko ya hifadhi za jamii” alisema Mbilimnyi.
Msemaji huyo
aliendelea kusema “Jambo hili ni jema sana na Kambi Rasmi ya Upinzani inaliunga
mkono”.
Kuanzishwa kwa Bodi
ya Ithibati pamoja na Baraza Huru la Habari ni jambo jema vitu ambavyo vitalinda
maslahi ya mwandishi wa habari kwa kuzingatia kuwa moja ya kazi Baraza na Bodi ni
kuweka viwango vya uangalizi pamoja na utaratibu wa kitaaluma katika kuratibu tasnia
ya habari nchini.
Mbilinyi ametoa rai
kwa Wabunge wote bila kujali itikadi za vyama kutambua kuwa jukumu la kutunga
sheria ni wajibu wao wa kikatiba ambayo wanawajibika wakiwa sehemu ya Bunge
kufanya kazi kwa maslahi mapana ya taifa.
Aidha, Mbilinyi
amesisitiza kuwa katika Mkutano wa Nne wa Bunge la 11 Septemba 15 mwaka huu,
Serikali ilileta Muswada wa Huduma za Habari na kusomwa mara ya kwanza kwa
lengo la kuwapa nafasi Wabunge pamoja na wadau mbalimbali wa habari kupitia na
kuufanyia tafakuri ya kina na hatimaye kutoa
ushauri kwa Serikali kuhusu Muswada huo.
Naye Wiziri wa
Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amesema kuwa mageuzi katika
tasnia ya habari nchini yataifanya kuwa taaluma kamili itakayowaletea heshima
wanahabari na taifa kwa ujumla.
Kupitishwa kwa
Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari itatoa wigo mpana kwa wanahabari
kutekeleza majukumu yao kw uhuru ya kukusanya, kuhariri na kuchapisha au kutangaza
habari.
Waziri Nape ameongeza
kuwa pamoja na maboresho mengi ya Muswada huo pia unzingatia suala la mitambo ya
kuchapisha magazeti na majarida nalo limepewa uzito unaostahili kwa kutohusika
moja kwa moja kwa kosa la gazeti ambalo limechapisha habari yenye makosa ya
kisheria dhidi ya watu au taasisi mbalimbali.
Akinukuu maneno
mbalimbali ya watu maarufu duniani juu ya masuala ya habari akiwemo Rais wa
Marekani Thomas Jefferson Januari 16, 1789, Rais wa zamani wa Afrika Kusini
Nelson Mandela, Muasisi wa Taifa la India Mahatma Ghandhi, Baba wa Uhuru wa
Habari John Stuart Mill (1806-1873) pamoja na Baba wa Taifa Mwalimu Julius
Nyerere, Waziri Nape alimesma kuwa mmoja wa viongozi hao Mahatma Ghandhi
aliamini kuwa uhuru wa kweli wa kujieleza ni ule unaoweka mbele heshima ya watu
wengine na kuwalinda dhidi ya dhara, kebehi, kejeli na madhara mengine huku
Baba wa Uhuru wa Habari John Stuart Mill akibainisha dhima ya uhuru wa vyombo
vya habari na umuhimu wa kuwa huriu unapaswa kuzingatia ukomo wa haki ya kupata
habari kuwa unakoma pale haki za watu wengine zinapoanzia.
Akichangia katika
mjadala wa Muswada huo wakati, Mbunge Sixtus Mapunda amesema kuwa kwa muda
mrefu tasnia ya habari haikuwahi kupata hadhi inayostahili ndani ya nchi pamoja
na kazi nzuri ya kuhabarisha, kufundisha, kukosoa na kuwasaidia watu watu wenye
matatizo wenye changamoto mbalimbali hata kufikia hadhi ya kuitwa muhimili wan
ne wa dola.
“Tasnia hii haikuwahi
kulindwa, tasnia hii haikuwahi kuenziwa, tasnia hii haikuwahi kuheshimiwa
inayostahili, kwa mwandishi wa habari mwenyewe, kwa chombo cha habari na
wamiliki wa chombo cha habari tofauti na tasnia nyingine nyingine, kwa mara ya
kwanza ndani ya nchi hii, heshima ya tasnia inapatikana” alisema Mapunda.
Mapunda ameitaja
tasni hizo kuwa ni za Madaktari, Wahasibu na Wahandisi ambao wanachombo chao
kinacholinda maslahi yao, maadili yao na kinachowalinda ili kuendelea kulinda
taaluma yao.
Aidha, Mapunda
amesema kuwa kwa miaka miaka zaidi ya 23, Muswada utasaidia kutatua matatizo
yote yaliyokuwa yanatokana na mapungufu ya Sheria ya Magazeti ya mwaka 1976 kwa
kuwa na Bodi ya Ithibati, Baraza Huru la Habari, Bodi ya Ithibati Mfuko wa
Mafunzo ambayo ni mambo mapya.
Zaidi ya hayo,
Mapunda aliongeza kuwa watu wenye vipaji vya kuandika habari kulingana na
taaluma zao ikiwemo uchumi hawajazuiliwa na Muswada wa Sheria ya Huduma za
Habari wa mwaka 2016.
Chimbuko la Muswada
huo linatokana na baadhi ya vipengele vya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania baada ya kufanyiwa marekebisho mwaka 1984 ambapo haki ya kikatiba ya
kutafuta, kupokea na kutoa habari imeainishwa kwenye Ibara ya 18 (b) pamoja na
mikataba mbalimbali ya kimataifa ya inayoainisha haki na wajibu wa sekta ya
habari.
Mikataba huyo ya
Kimataifa ni pamoja na ule wa Haki za Kisiasa na Kiraia wa mwaka 1966 ambao Tanzania
iliuridhia Juni 11, 1984 pamoja na Mkataba wa Afrika wa Haki za Binadamu na
Watu 1981 ambao nao uliridhiwa Februari 18, 1984.
0 maoni:
Chapisha Maoni