Balozi wa Falme za nchi za Kiarabu nchini Tanzania Mhe. Abdulla Al Suwaid mapema leo  Novemba 4.2016 amemtembelea Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu na kufanya mazungumzo. Moja ya mazungumzo waliyoongea ni pamoja na kuimarisha sekta ya afya ikiwemo ya kubadilishana kitaalam kwa kubadilishana ujuzi kwa madaktari wa nchi zote mbili
Aidha Waziri Ummy alimtaka Balozi huyo kusaidia Wilaya ambazo mapato yake ni kidogo na hawana hospitali za wilaya kuweza kuwajengea pamoja na kusaidia vifaa na vifaa tiba na masuala ya afya ya mama na motto nchini.
Hata hivyo Balozi Al Suwaid ameahidi kuisaidia Tanzania katika maeneyo yote aliyoyainisha Waziri pamoja na kuboresha hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma na ile ya matibabu ya Moyo ya Jakaya Kikwete.
Licha ya hivyp Balozi hiyo wamejenga kituo cha afya cha Waso kilichopo Wilayani Ngorongoro
Ummy Mwalimu BaloziBalozi wa Falme za nchi za Kiarabu nchini Tanzania Mhe. Abdulla Al Suwaid  akizungumza na Waziri wa Afya, maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto Mhe. Ummy Mwalimu alipomtembelea ofisini kwake leo Novemba 4.2016