Ijumaa, 4 Novemba 2016

Qatar kushirikiana na Tanzania katika sekta ya Afya

Posted by Esta Malibiche on News

Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu amekutana na kufanya mazungumzo na Balozi wa Qatar , Balozi Abdullah Al Maadadi ofisini kwake na kuzungumza kuhusu masuala ya sekta ya afya.
Katika mazungumzo hayo Waziri wa Afya mhe Ummy Mwalimu amemuomba Balozi wa Qatar kuishawishi Serikali yake kuanzisha Ushirikiano rasmi kati ya nchi hizi mbili katika Sekta ya Afya kwa kusaini Hati ya Makubaliano ya Kushirikiana.
Mhe Balozi amekubali Ombi la Mhe Waziri kwa kuahidi kulifanyia kazi.  Ambapo maeneo ya ushirikiano ikiwemo kubadilishana kujenga uwezo wa Rasilimali Watu ikiwemo kubadilishana Wataalam na kuimarisha huduma za Afya ya Uzazi na Mtoto ikiwemo upatikanaji wa Vifaa na Vifaa Tiba
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu akisalimiana na  Balozi wa Qatar , Balozi Abdullah Al Maadadi.
Ummy Mwalimu QatarWaziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na watoto Mh. Ummy Mwalimu akifanya mazungumzo na  Balozi wa Qatar , Balozi Abdullah Al Maadadi.

0 maoni:

Chapisha Maoni