Posted by Esta Malibiche on Nov7,2016 in NEWS
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi Mhe. Hamadi Massauni akijibu hoja mbalimbali za wabunge katika
mkutano watano wa Bunge la 11 linaloebdelea Mjini Dodoma Novemba 7,
2016.
……………………………………………………….
Na Jacquiline Mrisho – Dodoma.
Jumla ya askari 152 wamefukuzwa
kazi mwaka huu na Jeshi la Polisi kwa sababu ya kukiuka Sheria, Taratibu
na Kanuni ya Jeshi hilo kama zilivyoainishwa katika Kanuni za Kudumu za
Polisi (PGO) namba 103.
Idadi ya askari hao waliofukuzwa
kazi imetolewa leo mjini Dodoma na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya
Nchi, Mhandisi Hamad Masauni alipokuwa akijibu swali la Mbunge wa Viti
Maalum Mhe. Maryam Msabaha aliyehitaji kufahamu juu ya idadi ya askari
waliochukuliwa hatua kwa sababu ya utovu wa nidhamu.
Mhandisi Masauni amesema kuwa
kazi ya Vikosi vya Ulinzi na Usalama ni kulinda raia, mali zao pamoja na
mipaka ya nchi lakini kuna baadhi ya askari hao wanakwenda kinyume na
Sheria kwa kuwapiga wananchi na kuwasababishia ulemavu pamoja na vifo
hivyo Jeshi hilo limewachukulia hatua za kinidhamu.
“Jeshi la Polisi hufanya kazi kwa
mujibu wa Sheria, Kanuni na Taratibu zilizopo lakini kuna baadhi ya
askari wamekuwa wakikiuka maadili na mwenendo mwema wa Jeshi letu hivyo
kuanzia Januari 2015 hadi Juni 2016 tuliwachukulia hatua za kinidhamu
askari 200”, alisema Mhandisi Masauni.
Naibu Waziri huyo amefafanua kuwa
baada ya askari hao kuchukuliwa hatua za kinidhamu, walifanyiwa
uchunguzi wa kina na jumla ya askari 152 kati ya 200 walikutwa na hatia
hivyo hatua iliyofata ni kuwafukuza kazi.
Akizungumzia kuhusu mpango wa
Serikali juu ya kujenga nyumba za askari Polisi, Mhandisi Masauni
amesema kuwa wanatambua tatizo la makazi ya Askari Polisi katika maeneo
mbalimbali nchini hususani kwenye mikoa mipya hivyo Serikali ina nia ya
kutatua tatizo hilo kwa kuanza ujenzi wa nyumba kwa ajili ya askari hao.
“Serikali imedhamiria kupunguza tatizo la upu
ngufu wa makazi ya askari polisi
kwa kujenga nyumba kwa awamu kupitia mpango wa ujenzi wa nyumba 4,136
nchi nzima ambao utaanza kutekelezwa baada ya taratibu za mkopo wa
kuwezesha ujenzi huu kukamilika”, aliongeza Mhandisi Masauni.
0 maoni:
Chapisha Maoni