Jumatatu, 7 Novemba 2016

LIGI YA WANAWAKE MCHEZO MMOJA TU

Posted by Esta Malibiche on Nov 7,2016 in MICHEZO

imagesRaundi ya Pili ya Duru la Kwanza ya Ligi Kuu ya Taifa ya Wanawake itaendela kesho Jumanne kwa mchezo mmoja tu, wa Panama ya Iringa kuwa wageni wa timu ya Marsh Academy kwenye Uwanja wa CCM Kirumba jijini Mwanza.
Lakini, wakati mchezo huo Na. 5 wa Kundi B, ukifanyika michezo mingine mitano ya raundi ya pili ikiwamo mitatu ya Kundi A, imebidi iahirishwe na itapangiwa tarehe nyingine. Sababu kubwa ya kuahirishwa kwa michezo hiyo ni uwingi wa wachezaji kutoka timu zinazoshiriki ligi hiyo kujumuishwa kwenye timu ya taifa ya Wanawake – Twiga Stars.
Kwa mujibu wa ratiba ya ligi hiyo, michezo ya Kundi B iliyoahirishwa ni kati ya Majengo Women ya Singida iliyokuwa icheza na Baobab ya Dpdoma kwenye Uwanja wa Namfua mjini Singida wakati mechi nyingine ni kati ya Victoria Queens ya Kegera iliyokuwa icheze na Sisters ya Kigoma – mchezo ulipangwa kufanyika Uwanja wa Katiba mjini Bukoba.
Michezo ya Kundi A iliyoahirishwa ni kati ya Fair Play ya Tanga iliyokuwa iikaribishe Mburahati Queens ya Dar es Salaam kesho Novemba 8, 2016 kwenye Uwanja wa Mkwakwani ilihali michezo mingine iliyoahirishwa ni ya Novemba 9, ambako JKT Queens ya Dar es Salaam ilikuwa icheze na Viva Queens kwenye Uwanja wa Uhuru, Dar es Salaam wakati Evergreen Queens na Mlandizi zilikuwa zitumie Uwanja wa Karume, Ilala kucheza mechi yao hiyo.

0 maoni:

Chapisha Maoni