Jumatatu, 4 Julai 2016

Vyama Vya Siasa Zanzibar Kuhakikiwa

Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Leo imekamilisha zoezi la kuhakiki vyama vya siasa 21 kwa upande wa Tanzania Bara . Zoezi la uhakiki wa vyama vya Siasa visiwani Zanzibar litaanza  Julai 11 mwaka huu.
Uhakiki wa Vyama utafanyika katika Ofisi za Vyama zilizopo Zanzibar kwa maana ya Unguja na Pemba, zoezi hilo litajumuisha uhakiki wa idadi ya wanachama ambao Chama cha Siasa kinapaswa kuwa nao kwa mujibu wa masharti yalipo kwenye Sheria ya Vyama vya Siasa yam waka 1992.
Ikumbukwe kuwa ,zoezi hili ni moja kati ya shughuli za kawaida za Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa ambalo hufanyika maramoja kila mwaka likilenga kufahamu utekelezaji wa masharti na matakwa ya sheria ya vyama vya siasa.
MSA1Bi. Esther Mwanri, Mwanansheria kutoka ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa (wa nne kutoka kushoto) akiwa katika picha ya pamoja na baadhi ya viongozi wa chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mara baada ya zoezi la uhakiki  katika ofisi iliyopo Kinondoni Jijini Dar es Salaam. stori & picha na :ORPP
MSA2Afisa Sheria kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini Bi. Monica Mwailolo (kushoto) akikagua taarifa za Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) wakati wa zoezi la uhakiki uliofanyika katika ofisi hiyo iliyopo Magomeni Jijini Dar es salaam, katikati ni Katibu Mkuu wa Chama cha Tanzania Labour Party (TLP) Bi. Nancy Mrikalia akifuatiwa na Mwenyekiti wa Chama hicho Bw. Augustine Mrema.
MSA3Willy Brown Nyantiga, Mhasibu kutoka Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini akielezea jambo wakati wa zoezi la uhakiki ulioanyika katika Ofisi za Chama cha Union for Multiparty Democracy (UMD). Kulia ni Mwenyekiti  Taifa wa chama hicho Bw.Kamana Masoud na  Kushoto ni Msajili Msaidizi wa Vyama vya Siasa” Gharama za Uchaguzi na Elimu kwa Umma”” Bibi. Piencia Kiure

WAKUU WAPYA WA WILAYA ZA MKOA WA MWANZA WAPEWA MAJUKUMU MARA BAADA YA KUAPISHWA.

Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, akizungumza katika hafla ya kuwaapisha wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza hii leo, Julai 04,2016 katika viunga vya ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza.
Na BMG
Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella, amewataka wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa huo kuhakikisha wanashirikiana na kamati za ulinzi na usalama pamoja na wananchi kwenye wilaya hizo ili kukomesha mauaji dhidi ya watu wenye
ulemavu wa ngozi na vikongwe yanayochangiwa na imani potofu za kishirikina.
Akizungumza baada ya kuwaapisha wakuu hao wa wilaya zote saba za mkoa wa Mwanza, Mongella amesema kwa muda mrefu mkoa wa Mwanza umekumbwa na matukio ya mauaji ya watu wenye ualbino na vikongwe kutokana na imani za kishirikina
na kwamba wakati umefika kuhakikisha matukio hayo yanakwisha.
Amesema mkoa huo umejipanga vyema kuhakikisha matukio hayo yanakuwa historia kwa kuwa hakuna binadamu mwenye mamlaka ya kutoa uhai wa binadamu mwenzake kwa sababu yoyote ile.
Mkuu huyo wa mkoa amewapa mwezi mmoja wakuu hao wapya wa wilaya kumaliza tatizo la madawati pamoja na kuwachukulia hatua watumishi hewa 1,057 waliogundulika kwenye wilaya zote za mkoa wa Mwanza.
Mongella amewata wakuu hao wa Wilaya kuhakikisha kwamba matumizi ya dawa za kulevya katika wilaya zao yanakomeshwa ambapo amepiga marufuku matumizi ya shisha katika hoteli na klabu zote za muziki pamoja uchezaji wa “pool table” na unywaji wa pombe saa za kazi huku akitanabaisha kwamba atakaeshindwa kutekeleza maagizo hayo ni dhahiri shahiri kwamba atakuwa ameshindwa kusimamia majukumu yake.
 
Aidha Mongella amemtaka mkuu wa Wilaya ya Nyamagana kuhakikisha kwamba hadi ifikapo Agosti mosi mwaka huu awe amewaondoa wafanyabiashara ndogondogo waliosambaa kwenye maeneo mbalimbali ya katikati ya jiji Mwanza.
 
Wakuu wapya wa Wilaya za Mkoa wa Mwanza walioapishwa, wamesema wamejipanga vyema kushirikiana na viongozi wengine pamoja na wananchi katika Wilaya zao ili kuhakikisha kwamba wanatekeleza vyema majukumu yao ikiwemo kuimarisha suala la ulinzi na usalama katika jamii.
Wakuu wapya wa Wilaya saba za Mkoa wa Mwanza walioapishwa hii leo ni Mary Onesmo Tesha wa Nyamagana, Estomin Francis Chang’a wa Ukerewe, Hadija Rashid Nyembo wa Magu,
Juma Samwel Sweda wa Misungwi, Emmanuel Enock Kipole wa Sengerema, Dkt.Leonard Moses Masale wa Ilemela na Mhandisi Mtemi Msafiri Simion wa Kwimba ambapo wote wamekabidhiwa vitendea kazi ikiwemo Katiba ya Tanzania pamoja na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2015/20.
Mkuu wa Wilaya ya Sengerema, Mh.Emmanuel Enock Kipole (kulia), akiapa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Mwanza, John Mongella (kushoto).
Mkuu wa Wilaya ya Ukerewe, Mhe.Estomin Francis Chang’a (kushoto) akiapa mbele ya mkuu wa mkoa wa Mwanza, Mhe.John Mongella (kulia).
Mkuu wa Wilaya ya Magu, Mhe.Hadija Rashid Nyembo, akiapa hii leo
Continue reading →

0 maoni:

Chapisha Maoni